Feb 1, 2011

BASATA kuwakutanisha wasanii wa Tanzania na wa nje

 Katibu Mtendaji wa Basata, Gonche Materego

 Sehemu ya umati wa washiriki wa Jukwaa la Sanaa, Basata

Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), linatarajia kuwakutanisha wasanii wa Tanzania na wasanii wa nje ili kubadilishana ujuzi na uzoefu utakaoitambulisha sanaa kwenye soko la kimataifa.

Akizungumza jijini Dar es Salaam kwenye Jukwaa la Sanaa Jumatatu wiki hii, Katibu Mtendaji wa Basata, Gonche Materego alisema kuwa, kuwakutanisha wasanii wa nchini na wale wa kutoka nje ya nchi hasa nchi jirani kutaweza kuleta mabadiliko makubwa katika tasnia ya sanaa.

Alisema kuwa nia nyingine ya kuwakutanisha wasanii hao ni kuhakikisha wanakuza vipaji kwa kiwango kikubwa kwa kushirikiana na wasanii mbalimbali.

“Tunataka sasa wakati ufike kwa wasanii nchini na sisi tujivunie chetu kupitia ujuzi na uzoefu kutoka kwa wasanii wenzetu kwa sababu sisi wenyewe ni mashahidi wa kazi zetu ambazo zimeonekana zikiiga mirindimo ya wenzetu,” alisema Materego.

Alisema katika kuhakikisha wanakabiliana na wizi wa kazi za wasanii nchini, baraza hilo linatarajia kukutanana mashirikisho ya wasanii, ili kujadiliana kuhusu kuondoa tatizo hilo.

No comments: