May 30, 2012

Ubora ndiyo suluhisho kwa kazi zetu kung’ara kimataifa


Filamu ya Senior Bachelor iliyopata tuzo katika
tamasha la filamu la Zanzibar (ZIFF) kupitia
kipengele maalum cha filamu za Tanzania.

Filamu ya Fake Pregnant

CHANGAMOTO kubwa ambayo imekuwa midomoni mwa wengi katika soko la filamu za Tanzania na hata Afrika kwa ujumla ni ile ya kuzalisha sinema zisizo na ubora unaoridhisha. Changamoto hii ambayo ni sehemu ya mambo ambayo yameonekana kuwa magumu kutatuliwa (crux) na ndiyo mjadala wangu wa leo, ni suala ambalo tuko nalo kwa muda mrefu sasa tangu sekta hii ya filamu nchini (Bongo movies) iwepo. 

Katika hatua hii, ni muhimu kutambua kuwa nakusudia kuelezea kwa kiasi kikubwa kutokana na mtazamo wa wangu kuhusu sekta ya filamu ya Tanzania, ambalo ndilo soko la filamu ninalolijua vizuri na nililolifanyia utafiti wa kutosha.

May 24, 2012

Soko huria na filamu za Bongo


Men's Day Out

Aching Heart

Glamour

Uchumi wa soko huria Bongo karibuni umechangia kukua kwa sinema  za Kiswahili. Ukipita mitaani Bongo unakutana na filamu kila kona. Si kama miaka ileeee… tukililia sinema hatuzioni… Imekuwa kama mchezo  bila refa, mkutano bila mwenyekiti, darasa bila mwalimu, nyumba bila mzazi…

Wafanyabiashara wanaahidi milioni kumi hadi ishirini kwa sinema; watoaji wanalipua; waigizaji hawalipwi vizuri; utengenezaji sinema unafanywa haraka haraka.  Sinema zinatolewa ndani ya mwezi mmoja. Haraka haraka…

May 22, 2012

Kwanini tuelendelee kuwa sekta ya 'kuganga njaa' tu?
Picha zote kwa hisani ya Mwewe

NILIANDIKA wakati wa msiba wa Kanumba kuwa umati wa watu waliojitokeza siku ya msiba wake ni ishara tosha kuwa sekta ya filamu nchini ni kubwa na yenye nguvu kubwa lakini iliyotelekezwa na serikali. Kama serikali itaamua kuzichukulia filamu kwa umakini mkubwa, ikaandaa sera na kuunda chombo maalum kitakachoshughulikia filamu mfano wa kile cha Afrika Kusini cha National Film and Video Foundation (NFVF), naamini kabisa zinaweza kuwa chanzo kikubwa na muhimu sana katika kujenga taifa na zinaweza kutumika kama jukwaa la kuchochea mijadala nchini kote.

Kupitia chombo chao cha NFVF Afrika Kusini wanajivunia ‘hazina’ za sekta ya filamu ya nchi hiyo kama Tsotsi, iliyoshinda tuzo ya Academy mwaka 2006, Yesterday, filamu nyingine iliyoshiriki tuzo za Oscar na iliyowahi kushinda katika tuzo mbalimbali za kimataifa, na U Carmen E Khayalitsha, iliyoshinda tuzo ya Golden Bear mwaka 2005 katika Tamasha la Filamu la Kimataifa la Berlin.

Muigizaji wa filamu ya Yesterday, Leleti Khumalo

Filamu ya Yesterday

Filamu ya Tsotsi iliyopata tuzo ya Oscar

Filamu hizi zimekuwa zikitia chachu na hamasa kwa watengenezaji wa filamu wa Afrika Kusini kuwa wabunifu na wenye kujali ubora. Vipi kuhusu sisi? Hivi serikali haidhani kuwa kuanzisha chombo cha aina hii kutasaidia kutufanya tuwe na kazi nzuri ambazo siku moja zinaweza kushinda tuzo katika matamasha makubwa na yanayoheshimika duniani?

Mbona hatujiulizi, sekta ya filamu Tanzania inatengeneza sinema nyingi mno zinazoifanya kushika nafasi ya tatu katika bara la Afrika, nyuma ya Nollywood (Nigeria na Ghana), lakini ni Afrika Kusini ambayo ina mafanikio makubwa kwenye sekta ya filamu. Kwa nini hatujiulizi kuwa sinema nyingi za bajeti kubwa na zenye mafanikio makubwa za kimataifa zimekuwa zikitengenezewa Afrika Kusini.

May 16, 2012

Tuache malumbano, tuunganishe nguvu kuikomboa sekta ya filamu


Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania, Simon Mwakifwamba

Baadhi ya wasanii wanaosemwa kuwa 
wanafanya vizuri kwenye soko la filamu nchini

SEKTA ya filamu ni moja ya sekta ambazo zimezongwa na matatizo makubwa. Tathmini nyingi zilizofanyika na zinazoendelea kufanyika zinabaini kuwa chanzo kikuu cha matatizo haya ni kutoeleweka kwa dhana nzima ya burudani hususan filamu, kutothaminiwa kwa filamu na kwa serikali kutokuwa na kipaumbele katika tasnia ya filamu katika mipango ya maendeleo ya nchi yetu.

Ingawa jamii na viogozi wa nchi yetu hawawezi kukwepa lawama kwa maendeleo hafifu ya sekta ya filamu na burudani kwa ujumla wake, wasanii, waandaaji na watendaji wengine katika sekta hii wanastahili kulaumiwa zaidi kwa kuwa hawafanyi jitihada za kutosha katika kuelimisha na kuwaelewesha wananchi juu ya dhana ya burudani (filamu), mchango wake katika uchumi, ajira na umuhimu wake katika kusimulia hadithi zetu.

May 11, 2012

Bila sera nzuri ya filamu hatufiki kokote


Dk. Fenella Mukangara, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo

NANI anaweza kunihakikishia kuwa tuna sera ya filamu? Je, sera ya filamu nchini ni ipi? Kama kweli tunaamini kuwa tasnia ya filamu ni moja ya sekta zenye nguvu na yenye kuchangia kwa kiwango kikubwa katika ajira kwa vijana, kwa nini hatuna sera inayotuongoza? Tutaendelea kuongozwa na matamko ya viongozi hadi lini? Ieleweke matamko si sheria, ndiyo maana kila kiongozi anayeingia anakuwa na matamko yake ambayo atakayefuata baada yake halazimiki kuyafuata.

Hivi hatuoni kama huu ni muda muafaka wa kuwa na sera ya filamu itakayotuongoza katika kutenda kazi zetu? Mbona kuna sera ya utamaduni japo hata huo utamaduni wenyewe unapuuzwa? Lakini ipo! Vipi kuhusu filamu?

May 8, 2012

Sajuki kwenda India leo


 Sadiki Juma Kilowoko (Sajuki) alivyo sasa

Sajuki wakati akiwa na afya njema

Msanii wa filamu nchini, Sadiki Juma Kilowoko (Sajuki) leo anasafirishwa kuelekea India kwa ajili ya matibabu baada ya kukamilika kwa asilimia kubwa ya michango iliyotolewa na wasanii na wadau mbalimbali wa tasnia ya filamu.

Msanii huyo ataongozana na watu wengine wawili katika safari yake hiyo. Zaidi ya Shilingi milioni 25 zilikuwa zikihitajika kwa ajili ya kumtibu msanii huyo ambapo pesa iliyopatikana ni milioni 16 pamoja na tiketi tatu za ndege. Hata hivyo michango mingine inazidi kuchangishwa na zitatumwa kwa ajili ya kuendelea na matibabu zaidi.

May 4, 2012

Zitto Kabwe, Halima Mdee na wasanii kibao ndani ya wimbo wa Sajuki


Sadik Juma Kilowoko Sajuki katika picha tofauti.
Kushoto alivyo sasa na kulia wakati akiwa mzima


Picha hizi zinawaonyesha Sajuki na mke wake
Wastara Juma katika hali ya furaha

Waheshimiwa wabunge wametoa track inayoenda kwa jina la "Nimepoteza Mboni Yangu" kwa ajili ya kuhamasisha kumchangia pesa za matibabu msanii Sadiki Juma Kilowoko maarufu kama Sajuki wimbo huu utaanza kusikika katika kituo cha Clouds FM.

Watu wamekuwa wakihamasishwa kuchangia kwa kutuma pesa kwenye Account No. 050000003047 AKIBA BANK, jina la mwenye account ni Wastara Juma ambaye ndiye mke wa Sajuki au watume pesa kupitia MPESA No. 0762189592.

May 2, 2012

Tujifunze kutoka sekta ya filamu ya Afrika Kusini


Mtendaji Mkuu mpya wa Taasisi ya Taifa ya Filamu na Video 
(NFVF) nchini Afrika Kusini, Zamantungwa (Zama) Mkosi

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo nchini
Tanzania, Dk. Emmanuel Nchimbi

SIKU zote nimekuwa nikiwasihi wale wote wanaopenda maendeleo ya tasnia ya filamu nchini kuuangalia mfumo unaotumiwa na nchi ya Afrika Kusini ili kuiboresha sekta ya filamu nchini. Nadhani sasa ni muda muafaka kuliangalia kwa mapana yake, hasa kipindi hiki tunapojiandaa kuandika katiba mpya.

Sekta ya filamu ya Afrika Kusini ni moja ya sekta za filamu mahiri duniani, ni sekta inayokua na kuzidisha ushindani katika anga za kimataifa. Watengenezaji wa filamu wa ndani na wa nje wanatumia fursa mbalimbali zilizopo; maeneo ya kipekee - na gharama nafuu za uzalishaji kutokana na kiwango kizuri cha pesa ya nchi hiyo dhidi ya dola ya Kimarekani, ambacho hufanya kuwepo unafuu wa hadi asilimia 40 katika kutengeneza filamu Afrika Kusini kuliko Ulaya au Marekani na unafuu wa hadi asilimia 20 zaidi kuliko Australia.