Nov 25, 2009

Tanzania, nchi ya amani...

UPANDE MMOJA UKO HIVI: 

Mwananchi kajipumzisha baada ya kazi nzito

Hii ni moja ya shule zetu za msingi zilizoko vijijini

Ndoa za mastaa zina nini?

Sauda Mwilima akimuuliza swali Ivony Cheryl maaruf kama Monalisa

Kumekuwa na minong'ono kuwa ndoa za mastaa  duniani (ikiwemo Tanzania) huwa hazidumu. Minong'ono hiyo imempelekea mtangazaji wa kipindi cha Mcheza Kwao cha Star TV, Sauda Mwilima kuwatafuta baadhi ya wasanii ili kupata undani wa sakata hili. Hii imetokea leo kwenye viwanja vya Basata wakati wasanii hao walipokuwa wakifuatilia hatma ya usajiri wa shirikisho lao.


Ndumbagwe Misayo (Thea) akihojiwa na Sauda Mwilima kuhusu ndoa za Mastaa kutodumu

Kuna nini Basata?

Naibu Katibu Mkuu wa TAFF, Simon Mwakifwamba akielezea jambo mbele ya Katibu Mtendaji wa Basata


Leo tarehe 25/Novemba/2009 ni siku ambayo wadau mbalimbali wa filamu, wakiwemo waandaaji, waandishi wa skripti, waigizaji, wapiga picha na wengineo waliamua kuwasindikiza viongozi wao wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) walioongozwa na makatibu Bishop Hiluka na Simon Mwakifwamba kwenda zilipo ofisi za Basata kwa ajili ya kujua hatma ya usajiri wa shirikisho, hii ni baada ya wadau hao kuchoshwa na longolongo za Basata ambazo zimeonekana kuwa na nia ya kuwadhoofisha.

Nov 15, 2009

Kumekucha Bonanza la Wadau wa Filamu viwanja vya Leaders Club

Bonanza la Wadau wa Filamu hapa Tanzania linalofanyika kila jumamosi kwenye viwanja vya Leaders Club, Kinondoni linazidi kunoga. Hapa ni baadhi ya picha za matukio mbalimbali zilizochukuliwa Jumamosi ya tarehe 14/11/09.

Msanii Maarufu wa Kaole, Mlopelo akijimwaga kusakata dansi na mwanadada.

Shirikisho la Filamu Tanzania na Mikakati mipya

Katibu Mkuu, Bishop Hiluka (anayeandika) akijadiliana jambo na Msaidizi wake, 
Simon Mwakifwamba (Jaspa) na mjumbe wa bodi Mike Sangu (aliyesimama) kabla ya mkutano kuanza.

Katika kuonesha kuwa Shirikisho la Watengeneza Filamu Tanzania (TAFF) linajizatiti katika kuhakikisha kuwa fani ya uigizaji wa filamu inasonga mbele, juzi lilifanya mkutano mkubwa na wadau wa filamu katika kuhimiza uanzishwaji wa vyama vya fani husika (kama Chama Cha Waigizaji, Chama Cha waongozaji, Chama Cha Waandishi wa Skripti, n.k).

Nov 5, 2009

Steps Entertainment waja na mikakati mizito 2010Kampuni ya usambazaji wa filamu za Kibongo ya Steps Entertainment imebuni mikakati mipya katika kuboresha soko la filamu hapa nchini. Mikakati hiyo itaanza mapema mwakani 2010 hivyo wadau wote wa filamu wakae mkao wa kula kwani hivi karibuni wataelewa ni mikakati gani hiyo.

Ray na Johari wanapogeuka Madaktari!

Ray (Vincent Kigosi) akitoa maelekezo kwa Johari (Blandina Chagula) kuhusiana na mgonjwa ambaye hayupo pichani

Hii picha na zingine hapa chini ni picha za baadhi ya Wasanii maarufu katika tasnia ya Filamu hapa Tanzania ambazo zimechukuliwa kutoka kwenye filamu moja inayoitwa Pesa (Shekeli) iliyoandaliwa na Kampuni ya Aminaah Entertainment. Sinema hii imekusanya mastaa kibao wa filamu za Kibongo kama vile Ray, Johari, Mainda, Biggie, Sajuki, John Lister, Kaike, na wengineo kibao.