Jul 28, 2011

TUJADILI: Upi mfumo unaotufaa wa usambazaji wa filamu zetu?

 Rais wa Shirikisho la Filamu nchini, Simon Mwakifwamba

IJUMAA iliyopita nilielezea udhaifu wa wasanii kutojitambua unaotokana na kulewa umaarufu, pia niliuliza swali kama sanaa zetu zilivyo leo zinaweka kumbukumbu nzuri itakayorithiwa na vizazi vijavyo na kuashiria historia inayolingana na mila na desturi nzuri za kizazi husika. Au kama tunaweka kumbukumbu potofu ya sanaa zetu na uasili wake kwa vizazi vijavyo?

Leo najaribu kuangalia kwa makini kuhusu mfumo wetu wa usambazaji wa kazi za sanaa (hasa filamu) kutokana na sababu kuu mbili: kwanza nimepokea meseji kadhaa za wasomaji mbalimbali zilizonisisitiza nieleze namna tunavyoweza kujikwamua katika usambazaji na namna gani tunaweza kufanikiwa kuondokana na uharamia wa kazi za sanaa.

Ili kudhibiti wizi wa kazi za wasanii: SERIKALI KUGHARAMIA HAKIGRAMU

 Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Adam Malima

Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Mkoa wa Mara, 
Ester Bulaya

Ili kukomesha vitendi vya wizi wa kazi za wasanii nchini, Serikali imetenga kiasi cha Sh. milioni 470 ili kufanikisha mpango wa utengenezwaji wa stika maalumu (Haki gramu) zitakazowekwa kwenye kanda za sauti (kaseti), video na CD ili kukomesha wizi wa kazi za wasanii. Serikali imesema kuwa itashirikiana na nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), na nchi za SADC katika kuandaa stika maalum kwa ajili ya kudhibiti uharamia huo.

Mpango huo wa serikali ulielezwa bungeni mjini Dodoma jana (Jumatano) na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Adam Malima kwa niaba ya Waziri wa Viwanda na Biashara wakati akijibu swali la mbunge wa viti maalumu (CCM), Ester Bulaya, aliyetaka kujua ni vipi serikali imejipanga kukomesha wizi wa kazi za wasanii.

Jul 26, 2011

Monalisa, msanii pekee wa Afrika Mashariki anayeshiriki tuzo za Nigeria Enterteinment Awards

 Yvonne Cherryl (Monalisa)

"FILAMU za Tanzania zinapendwa sana nchi za nje, lakini katika utafiti wangu nimegundua hatuna wasambazaji ambao wanatusaidia kuzifikisha huko" ni maneno ya muigizaji mahiri katika tasnia ya filamu hapa nchini Yvonne Cherryl anayefahamika zaidi kama Monalisa.

Monalisa ambaye hivi sasa amechaguliwa kushiriki katika tuzo za NEA Awards (Nigeria Enterteinment Awards) zinazotarajiwa kufanyika nchini Marekani mwezi Septemba mwaka huu, anasema kuwa bado hakuna wasambazaji ambao wamejitolea kupeleka kazi za filamu nje ya nchi.

Jul 21, 2011

Hivi ni wasanii wangapi wanaoijua thamani yao?

 Msanii Aunt Ezekiel akiwa kwenye pozi

 Miriam Jolwa (Kabula) na Jacky Pentezel

HAKUNA ubishi kwamba, miongoni mwa fani mbalimbali za sanaa katika jamii ya Kitanzania kwa zama hizi, ni sanaa ya maigizo, hasa filamu ndiyo inayoonekana kutesa zaidi. Pamoja na sanaa ya filamu, pia sanaa ya muziki, hasa wa kizazi kipya imeonekana kutingisha miongoni mwa vijana.

Sanaa ya filamu hapa nchini imetokea kujitwalia wapenzi kibao kiasi cha kuwa kimbilio la vijana wengi, wake kwa waume, watoto kwa wakubwa na hivyo kuonekana kuwa mkombozi wa ajira kwa vijana hao huku wengi wakiwapongeza waigizaji wake kuwa, wameweza kuipa jamii ya Kitanzania kitu kipya.

Jul 20, 2011

Tulianza kwa kuiga stori, sasa tunaiga majina ya filamu za Kiingereza, sijui baadaye tutaiga nini?


Tasnia ya filamu Bongo ambayo ipo katika nchi ya Waswahili wanaozungumza Kiswahili fasaha lakini inayoongoza kwa kuwa na majina mengi ya Kiingereza kwenye sinema zake! Bahati mbaya majina haya ya filamu tunayoyatumia tayari yameshatumika kwenye filamu za nchi zingine zilizoendelea zinazozungumza Kiingereza.

Filamu za Bongo nyingi zinaaminika kukopi hadithi na visa vya filamu zingine za nje, lakini hata hili la majina nalo limekuwa ni kitu cha kawaida jambo linalotuletea aibu kubwa miongoni mwa mataifa mengine. Hebu angalia mfano mdogo hapa chini:

Deception

Wicked Love

This Is It

The Best Man


Offside

What Is It?
Hizi ni baadhi ya filamu ambazo tumeiga majina...
 

Jul 14, 2011

Kwa hili la Komedi tunaendelea kuonesha tusivyo na ubunifu!

 Lucas Mhuvile (Joti)

Ramadhani mwinshehe (Kingwendu)
NAKUMBUKA kabla ya teknolojia hii ya televisheni kuingia nchini mwetu kwenye miaka mwishoni mwa tisini, tulizoea kusikiliza michezo ya kuigiza na vichekesho kupitia redio, michezo kama vile Mahoka, Pwagu na Pwaguzi, Twende na Wakati na kadhalika. Wakati huo kituo cha redio kikiwa kimoja tu, yaani Radio Tanzania Dar es Salaam (RTD).

Ndipo miaka ya tisini vituo vingine vya redio vilipojitokeza na kuanza kutoa burudani huku vikimaliza ukiritimba wa RTD wa kuhodhi matangazo yote na kutulazimisha kusikiliza hata vile vipindi ambavyo hatukuvihitaji. Kuingia kwa redio zingine kulisababisha baadhi ya vituo hivi vipya kuwanyakua baadhi ya watangazaji waliokuwa RTD.

Jul 12, 2011

Nguvu zote za Bongo movie Club kuchaguana kumbe timu si yao!

Timu ya Bongo Movie

 Jacob Steven (JB), mwenyekiti mpya wa Bongo Movie Club

Kwa miezi kadhaa sasa tangu ile mechi ya hisani ya kwachangia waathirika wa Mabomu ya Mbagala kati ya Bongo Movie na Bongo Fleva kumekuwepo mtafaruku kati ya Bongo Movie Club na Shirikisho la filamu Tanzania (Tanzania Film Federation, TAFF), mtafaruku ambao ulitawala katika vyombo vya habari.

Kuundwa kwa Timu hii ilionekana kama ni kulipinga Shirikisho la Filamu, lakini wahusika wa Timu hii wakidai kuwa hakuna kitu kama hicho huku wakisisitiza kwamba Club hii iliundwa kwa ajili ya kufanya mazoezi kwa ajili ya Afya za Wasanii, na walio upande wa pili wakisema kuwa Bongo Movie Club ni Waasi.

Jul 11, 2011

Jacqueline Wolper azua tafrani mkutano wa Shirikisho la Filamu Tanzania

Jacqueline Wolper 


Baada ya Jacqueline Wolper kuzua tafrani 
wasanii wengine nao waliporomosha matusi.

Rais wa TAFF, Simon Mwakifwamba akionesha
magazeti yenye habari za ngono za waigizaji,
kulia kwake ni Kulwa Kikumba (Dude)

Steve Nyerere naye akitaka kupanda jukwaani 
kabla hajazuiwa na Rado

Mkutano mkubwa wa waigizaji na wadau wa filamu uliofanyika kwenye viwanja vya Leader Club Ijumaa ya tarehe 8 Julai, 2011, chini ya Shirikisho la Filamu Tanzania (Taff) ulisababisha tafrani kubwa baada ya muigizaji wa filamu, Jacqueline Wolper, ambaye pamoja na wasanii wengine nyota walihudhuria, alitoka toka sehemu aliyokuwepo na kuelekea jukwaani kwa spidi kwa ajili ya kumkwida Rais wa Shirikisho hilo, Simon Mwakifwamba (Jaspa), lakini Mabaunsa pamoja na askari walifanikiwa kumzuia ili asipande Jukwaa hilo.

Sababu ya Jack kutaka kumvamia Mwakifwamba ni baada ya Rais huyo kukemea na kutoa magazeti kadhaa ambayo yameripoti habari zinazohusiana na mambo ya ngono kwa baadhi ya wasanii hao.

Jul 8, 2011

Hoja za uongo kuhusu soko la filamu za Bongo

Elizabeth Michael maarufu kama Lulu, kushoto 
na msanii mwenzake maaruf kama Mikogo
wakijiandaa kwa filamu

Elizabeth Michael (Lulu) katika pozi


Wasanii Irene Uwoya na JB katika moja ya scene
za mapenzi kwenye filamu za Bongo

TUNAPOFIKIRIA juu ya faida na vikwazo vya kutatua matatizo ya uratibu wa jamii kupitia taratibu za masoko ya filamu, ni muhimu kuzitupilia mbali baadhi ya hoja za uongo zinazolazimishwa miongoni mwetu. Ninaposema hoja za uongo nakusudia maneno ambayo kutokana na ukweli ulio dhahiri hupita hivihivi bila hata ya kuwa na haja ya kuhoji au kuhitaji uthibitisho.

Ni maneno unayoweza kuyasikia kutoka kwa watu mbalimbali kuhalalisha kile wanachokiamini au wanachotaka jamii ikikubali kwa maslahi fulanifulani. Maneno ambayo hurudiwarudiwa kana kwamba ndiyo aina mojawapo ya maneno ya hekima. Hatari iliyoko ni kwamba, kwa sababu yameenea sana, hayafanyiwi uchunguzi wa kina. Na hicho ndicho ninachokusudia kukifanya leo.