Bayport

Bayport

fofam

fofam

imetosha

imetosha

Ads

Ads

Dec 31, 2017

Mwaka 2017 umekwisha, dira ya wasanii ni ipi?

Wasanii mbalimbali wakifuatilia mjadala kwenye ukumbi wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA)

Msanii akipiga tarumbeta

HEBU fikiria, unaamka asubuhi na mapema, unajiandaa na kubeba begi lako kisha unaelekea kituo cha basi, unalikuta gari na kupanda, lakini hujui unaelekea wapi!

Au mpo katika kituo cha mabasi, mara basi linakuja, kila mmoja analikimbilia na kupanda, tena mnafikia hatua ya kugombea siti, na safari inapoanza ndipo mnagundua kuwa gari haliendi kule mnakokwenda. Mnataharuki na kuanza kumpigia kelele dereva kumtaka asimamishe gari!

Dereva anawashangaa na analiegesha gari pembeni, kisha anawauliza kwani ninyi mnaelekea wapi? Hapo ndipo mnapojigundua kuwa kila mmoja anaelekea sehemu tofauti kabisa na linakokwenda gari!

Oct 23, 2017

Wasanii vunjeni ukuta wa fikra

Peter Tosh
Filamu ya Off Side
“EVERYBODY want to go to heaven, but nobody want to die…” hii ni nukuu kutoka kwenye wimbo wa Equal Rights wa aliyekuwa mwanamuziki mahiri wa reggae duniani, Peter Tosh. Maneno hayo ambayo tafsiri yake kwa lugha ya Kiswahili ni “Kila mtu anataka kwenda peponi, lakini hakuna anayetaka kufa…”

Sikuwa shabiki wa muziki wa reggae, ila nilipolazimika kusikiliza reggae nilipenda nyimbo za Lucky Dube na Peter Tosh. Wanamuziki wote wawili kwa sasa ni marehemu.

Ukiusikiliza kwa makini ujumbe ndani ya wimbo wa Equal Rights, utagundua kuwa ni chemsha bongo ya aina fulani. Maneno ya Peter Tosh katika wimbo huu yanaakisi hali halisi ilivyo katika shughuli za sanaa Tanzania, hasa muziki na filamu.

Muziki wa Singeli: ni mapinduzi mapya au kifo cha muziki?

Mwanamuziki Msaga Sumu

Mwanamuziki Sholo Mwamba
MUZIKI wa Tanzania unabadilika sana, wasanii wengi wamekuwa wakibuni mitindo ya aina mbalimbali ili kuzifanya kazi zao ziende mbali na kuvuta mashabiki wa muziki nchini na duniani kwa ujumla.

Miaka ya nyuma muziki wa dansi ndiyo ulikuwa ulishika hatamu, muziki huu ulioanza kama klabu ambapo watu walialikana kucheza aina mbalimbali za muziki wa kizungu mtindo maarufu uliojulikana kama ballroom dancing. Kisha taratibu ukaumbika ukifuata muziki wa soukous kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (rumba ya Kikongo) na tokea hapo ikawa inaitwa ‘rumba ya Tanzania’.

Oct 14, 2017

Miaka 18 baada ya kifo cha Mwalimu Julius K. Nyerere: Je, tunalinda utamaduni wetu kama alivyoamini?


LEO tunaadhimisha kumbukumbu ya miaka 18 tangu Baba wa Taifa na muasisi wa taifa hili, Rais wa kwanza wa Tanzania, Hayati Mwalimu Julius Nyerere aliyefariki dunia Oktoba 14, 1999 jijini London, Uingereza na kuzikwa Butiama, kijiji alichozaliwa.

Mwalimu Nyerere alikuwa kati ya viongozi wachache wa Afrika walioacha mwangwi katika utamaduni wa nchi zao.

Nyerere alikuwa mwalimu. Ni sahihi kusema silika ya ualimu iliathiri siasa na matendo ya Mwalimu Nyerere kama kiongozi wa Tanganyika na baadaye Tanzania. Aliiona nchi yake kama darasa na daima alikuwa akiwafundisha watu.

Sep 8, 2017

Madhara Yanayosababishwa na PonografiaMAPOKEO ya kazi za sanaa katika jamii yoyote hufuata utaratibu wa kurithisha mfumo, mtindo, muundo, maudhui na hivyo hubaki kuelezea juhudi, matatizo au mafanikio ya jamii husika.

Kama sanaa zenu haziakisi maisha yenu, basi mjue kuwa vizazi vyenu vitarithi mambo yasiyokuwa yenu. Sanaa kama nguzo mojawapo muhimu ya Utamaduni hukua na pia hufa.
Unaweza kujiuliza; Je, filamu zetu zilivyo leo zinaweka kumbukumbu nzuri itakayorithiwa na vizazi vijavyo? Au kizazi chetu kinaweka kumbukumbu potofu ya filamu na sanaa zetu na utamaduni kwa vizazi vijavyo?

Jul 27, 2017

Hakuna shaka Tanga ndio kitovu cha burudani TanzaniaNAUKUBALI sana mkoa wa Tanga, una historia nzuri katika burudani na unaaminika kuwa ndio kitovu cha burudani katika nchi hii, kuanzia kabumbu, muziki, sinema na kadhalika. Tanga ni jiji lililo ufukoni mwa Bahari ya Hindi.

Jina la mji wa Tanga linaaminiwa kutokana na neno “tanga” yaani kitambaa kikubwa kinachokingamishwa kwenye mlingoti wa jahazi, ilipewa jina hilo kwa sababu kisiwa cha Toten ilipo hori ya Tanga kina umbo linalofanana na kitambaa cha aina hii.

Jul 18, 2017

SRIDEVI KAPOOR: Supastaa wa kwanza mwanamke Bollywood

Sridevi Kapoor
TASNIA ya filamu ya India maarufu kwa jina la ‘Bollywood’ hadi sasa imekwisha tengeneza mastaa wengi wakubwa waliojulikana duniani, wakatengeneza pesa nyingi na kupata heshima kubwa ndani ya India na hadi nje ya mipaka ya India. Kwa mpenzi yeyote wa sinema, iwe ni sinema za Hollywood (tasnia ya sinema ya Marekani), au Nollywood (tasnia ya sinema ya Nigeria) bado atakuwa amekwishaziona filamu za India.

Nollywood mara nyingi wamekuwa wakiiga kutoka Bollywood, tasnia ambayo imewatengeneza waigizaji maarufu duniani kama Amitabh Bachchan, Shahrukh Khan, Aamir Khan, Salman Khan, Dilip Kumar, Raj Kapoor, Dharmendra, Hrithik Roshan, Rish Kapoor na wengine wengi kwa upande wa wanaume.