Dec 29, 2010

Soko la filamu Tanzania linakua? (3)

 Jengo la Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

 Aliyekuwa Naibu Wizara wa Habari Utamaduni na Michezo, 
Joel Nkaya Bendera akisisitiza jambo

*Watazamaji wa kazi za Kiswahili walihamasika zaidi baada ya ITV kurusha mchezo wa Tausi
*Serikali imekusanya sh. Bilioni 2 kwa mwaka 2005 hadi Mei 2009.

BURUDANI nchini Tanzania imepitia mabadiliko makubwa hadi kufika hapa ilipo. Kipindi kile, enzi za kina Black Moses, Maneno Ngedere, Bob Tiger na wengine wengi burudani ya disko ndiyo iliyoshika hatamu. Kipindi hicho ndipo hata zile sinema za kwenye majumba ya sinema (Avalon, Drive Inn Cinema, Empire, Starlight na kadhalika) zilikuwa zimeshika hatamu.

Dec 24, 2010

Vita ya wakoloni dhidi ya utamaduni wetu

Ramani ya bara la Afrika
 Moja ya sanaa za Kiafrika

HISTORIA ya ukoloni katika Bara la Afrika, inaonyesha jinsi walivyojitahidi kuua utamaduni wa Waafrika na kuwajenga katika misingi ya utamaduni wa kizungu. Katika baadhi ya makoloni, ubora wa Mwafrika ulipimwa kwa kiasi ambacho alikuwa amejengeka katika utamaduni huo.

Baadhi ya Waafrika waliweza hata kupewa uraia wa nchi za wakoloni kutokana na vile walivyokuwa wamejiimarisha katika  ‘ustaarabu’ wa wakoloni. Mchakato wa elimu haukuwa na maana tu ya kuwapatia Waafrika maarifa na ujuzi, bali pia ilikuwa ni fursa ya kuwaondoa katika utamaduni wao na kuwajenga katika utamaduni wa kizungu.

Sanaa na utamaduni wa Tanzania vithaminiwe

Rais Jakaya Kikwete akipiga ngoma ya kisukuma, 
moja ya tamadauni za Kitanzania 

 Kingo, moja ya majarida ya Kitanzania. 
Hapa alikuwa akitafuta Miss Tanzania wa ukweli

KADRI miaka inavyozidi kusonga mbele, ndivyo mabadiliko ya sayansi na teknolojia yanavyoongezeka nchini Tanzania, pia ndivyo jamii inavyosahau utamaduni wao kwa kuiga utamaduni wa kigeni ambao ingawa una faida, lakini matatizo ni makubwa zaidi. 
 
Tangu utandawazi ulipoanza kushamiri katika miaka ya 2000, ndivyo uigaji wa utamaduni kutoka mataifa mengine ya nje, nao uliingia kwa kasi nchini Tanzania, ambapo wananchi wengi nchini Tanzania waliacha utamaduni wao na kuiga wa nje.

Dec 21, 2010

Soko la filamu Tanzania linakua? (2)

Kava la filamu ya Aunt Suzzy, moja ya kazi za Kitanzania

Msanii wa filamu za Kibongo maaruf kama Kishoka

MWAKA 1945, baada ya Vita Kuu ya Pili, uoneshaji na usambazaji wa sinema ulibadilika kidogo kwenye baadhi ya sinema. Sinema kama “Mister English at Home” na “An African in London” zilitengenezwa kutufundisha mambo na tamaduni za Kiingereza. Hata sinema zilizoanza kutengenezwa nchini baadaye zilizingatia mambo kadha wa kadha kama; faida ya dawa (tiba) za Kimagharibi dhidi ya tiba za Kiafrika.

Waafrika katika filamu za Wazungu walifanywa waonekane (na bado wanaonekana) washenzi, watu wa chini, wafungwa, nk. Wakati mwingine walifanywa waonekane wakatili sana na wanaoamini mambo ya kishirikina.

Dec 15, 2010

Changamoto yatolewa kwa wasanii kuthamini kazi zao

Vincent Kigosi (Ray)

Emmanuel Myamba maaruf kama Pastor Myamba
 Jalida la Baab Kubwa linalopamba 
kichwa cha habari kuhusu wasanii matajiri

Wasanii nchini wameshauriwa kuthamini na kuheshimu kazi zao za sanaa ili ziweze kuwakomboa kiuchumi na kutokuwa tegemezi. Kauli hii imetolewa na Ofisa Utamaduni wa jiji la Mwanza, Rosemary Makenke alipokuwa akiwasilisha mada iitwayo "Sanaa ni Ajira, Tuithamini" kwenye Kikao cha Nane cha Sekta ya Utamaduni kilichofanyika jijini Mwanza.

Ofia Utamaduni huyo alisema kuwa wasanii sharti wajiheshimu wao na kazi zao za sanaa wanazozifanya katika jamii kwa kuwa kazi ya sanaa kwa sasa ni ajira. Pia alisema kuwa sheria ya hakimiliki bado haisimamiwi kikamilifu na kwamba jasho na kazi za wasanii zinaendelea kuporwa na wajanja wachache kila siku.
katika kikao hicho pia kilihudhuriwa na wasanii maaruf, Jacob Stephen maaruf kama JB na Mrisho Mpoto "Mjomba" ambao walikuwa kivutio kwenye mkutano huo.

BASATA yasema kuwa usajiri wa wasanii ndiyo mwanzo wa heshima katika sanaa

Sehemu ya jiji la Mwanza kilipofanyika Kikao cha nane cha Sekta ya Utamaduni

 
Mtendaji Mkuu wa Basata, Ghonche Materego
 
Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), Ghonche Materego amesema kwamba zoezi la usajili wa wadau wa sanaa linaloendelea nchini kote ni mwanzo wa kujenga heshima ya tasnia ya sanaa ambayo kwa miaka mingi imekuwa ikionekana kama ridhaa, isiyo na mchango wowote katika uchumi wa nchi na zaidi ya burudani tu.

Aliyasema hayo alipokuwa akizungumza kwenye Kikao cha nane cha Sekta ya Utamaduni kilichofanyika jijini Mwanza. Materego alisema kwamba, ni vema wasanii, wamiliki wa kumbi za sanaa na utamaduni na wadau wote wanaojihusisha na sekta ya sanaa

Kikao cha Nane cha Sekta ya Utamaduni kimefanyika Mkoani Mwanza

Jengo la PPF ndani ya ROCK CITY

Prof. Hermans Mwansoko na Gonche Materego
Kikao cha nane cha sekta ya Utamaduni kilifanyika jijini Mwanza hivi karibuni kikiwashirikisha wakurugenzi wa idara, maafisa utamaduni wote nchini na wadau mbalimbali wa utamaduni na kuja na mikakati mbalimbali ya uboreshaji.

Mkurugenzi wa Idara ya Utamaduni, Profesa Hermans Mwansoko alisema kikao hicho kilichobeba kaulimbiu ya Sanaa ni Ajira Tuithamini, kikajikita kwenye uwasilishaji wa mada na machapisho mbalimbali kuhusu sekta ya utamaduni ambapo wajumbe walipata fursa ya kujadili, kuja na changamoto mbalimbali na baadaye kupata majibu na dira ya changamoto hizo.

Soko la filamu Tanzania linakua?

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitafakari

TASNIA ya filamu hapa Tanzania kwa miaka ya karibuni imeonekana kupata mwamko mkubwa sana, lakini kwa bahati mbaya (au kwa makusudi) mara nyingi kumekuwa hakuna takwimu au taarifa sahihi kuhusu mwamko na maendeleo ya tasnia hii ya filamu hapa Tanzania.

Miaka michache iliyopita asilimia kubwa ya Watanzania walipendelea kutazama filamu zilizotoka nje ya nchi, hususan sinema za Nigeria na India, lakini hivi sasa hali imekuwa tofauti kidogo. Tofauti hiyo imesababishwa na ujio wa hizi filamu za Kibongo za kizazi kipya (new generation films), kutoka kwa wasanii na waandaaji wa Kitanzania ambao mpaka sasa wamechangia kwa kiasi kikubwa kuitambulisha tasnia ya filamu Tanzania ndani na nje ya mipaka ya nchi.

Dec 7, 2010

HISTORIA YA FILAMU (4): Kukua kwa biashara ya Sinema Duniani

Edwin S. Porter - The Great Train Robbery (1903)

George Melies

KAMA nilivyoanza kuelezea issue iliyopita, biashara ya sinema ilianza kujikita rasmi na kuwa ajira kamili iliyowawezesha watu kujipatia kipato halali kutokana na kazi hiyo.

Kukua kwa sekta ya filamu kulikoambatana na biashara hakukuanza hivi hivi tu, kulitokana na changamoto nyingi sana na kulianza kuonekana kwa Georges Mèliès wa Paris, Ufaransa aliyepiga picha na kufanya maonesho ya filamu (film exhibition) mwaka 1896. Kazi zake kama “A TRIP TO THE MOON (1902)”, kazi inayosadikiwa kuwa ndiyo iliyoanzisha vuguvugu na kutia hamasa (potray) kwa wanasayansi kuhusu safari za angani (space travel).

Dec 1, 2010

HISTORIA YA FILAMU (3): Mwanzo wa Sinema za Sauti (Sound Era)

 Humphrey Bogart, muigizaji anayeshika namba moja ya ubora katika historia

MAJARIBIO ya kuchanganya muziki kwenye sinema kwa kutumia njia mbalimbali hatimaye yalifanikiwa; kurekodi moja kwa moja au kuingizia muziki studio (play back) wakati wa uhariri, ingawa juhudi zilianza tangu kipindi chote tangu mwanzo wa sinema bubu, lakini matatizo makubwa mawili (twin problems) ya kuoanisha (synchronise) na kukuza (amplifiy) sauti katika kiwango kinachostahili yalikuwa kikwazo kikubwa (Eyman, 1997).

Mwaka 1926, studio ya Warner Bros ya Hollywood ilitambulisha mfumo mpya uliojulikana kama ‘Vitaphone’, kwa kutoa sinema fupi zilizotokana na matukio ya moja kwa moja (live entertainment acts) ya wasanii maarufu na baadaye kuongezea sauti maalum (sound effects) na muziki (orchestral scores).