Jun 30, 2011

Mafunzo ni muhimu katika tasnia ya filamu

Moja ya mafunzo ya filamu yaliyotolewa hapa nchini. 
Hapa washiriki wakibadilishana mawazo nje ya 
Kituo cha Utamaduni cha Ujerumani (Goethe Institut). 
Kulia ni mwandishi wa makala hii, Bishop Hiluka

MWISHONI mwa wiki iliyopita Tamasha la Filamu za Nchi za Majahazi (ZIFF 2010), lilihitimishwa huku kukiwa na mambo kadhaa yanayozidi kuitia doa tasnia ya filamu nchini. Katika tamasha hilo filamu zaidi ya 100 zilioneshwa sambamba na wasanii mbalimbali kutoka nchini Tanzania, Afrika na nje ya Afrika kuonesha burudani ndani ya Visiwa vya Zanzibar.

Tamasha hilo la filamu la Zanzibar lililoanza Juni 18 ndani ya Ngome Kongwe Zanzibar, likiwa linafanyika kwa mara ya 14 tokea lilipoanzishwa, limekuwa na mchango mzuri sana katika tasnia ya filamu na linapaswa kuchukuliwa kama somo muhimu sana na waigizaji, waandaaji, waongozaji na watunzi wa filamu wa Tanzania.

Jun 24, 2011

Tamasha la filamu: “Grand Malt Tanzania Open Film Festival” ndani ya Tanga kuanza Juni 27

Mkurugenzi wa Sofia Production, Mussa Kissoky (kulia)
akielezea kwenye ukumbi wa Habari MAELEZO.
Katikati ni Meneja Masoko wa TBL, Fimbo Butallah,
kushoto ni Meneja wa Grand Malt, Consolata Adam

Tamasha kubwa la wazi la filamu nchini Tanzania litakalojulikana kama 'Grand Malt Tanzania Open Film Festival' linatarajiwa kufanyika jijini Tanga kuanzia Juni 27, 2011 ambapo zaidi ya Filamu kumi kali kutoka kwa watayarishaji mahiri wa Tanzania zinatarajiwa kuoneshwa katika tamasha hilo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa kampuni ya
Sofia Production, Mussa Kisoki alisema tamasha hilo litafanyika katika viwanja vya Tangamano, kuanzia Juni 27 na kumalizika Julai 3 mwaka huu.

Channel mpya ya Kiswahili yazinduliwa na M-net Afrika jijini Dar es Salaam

 
Mkurugenzi Mtendaji wa M-Net Africa, Bilola Arabi
akizungumza wakati wa uzinduzi

Muigizaji maaruf wa Tanzania, Steven Kanumba 
akichanagia wakati wa uzinduzi


Juzi jioni, 22 Juni, 2011 kulifanyika uzinduzi wa channel mpya ya Kiswahili (Africa Magic Swahili) uliofanywa ndani ya hoteli ya Movenpick ya  jijini Dar es Salaam, Channel hiyo inatarajiwa kuanza kuruka hewani kuanzia Julai mosi, 2011, ambapo filamu za Bongo zitapata nafasi kubwa ya kuonekana kwenye channel hiyo.  Pia imebainika kuwa channel hiyo itakuwa ikirusha matangazo yake katika nchi zinazoongea Kiswahili ikiwemo Kenya, Uganda, Rwanda, Ethiopia, Burundi, Congo pamoja na DRC.

Waziri Nchimbi, ni kweli wasanii hawapatani, sasa?

 Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, 
Emmanuel Nchimbi

Dilesh Solank, Mkurugenzi wa Steps Entertainment, 
wasambazaji wa filamu nchini wanaolalamikiwa 
kuasisi mgawanyiko wa wasanii

WIKI iliyopita, wasanii wa filamu walio chini ya mwamvuli wa Bongo Movie Club walizuru Bungeni Dodoma, walikocheza mechi ya kirafiki na timu ya wabunge, Bunge Sports Club. Ni katika hafla hiyo Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Emmanuel Nchimbi, alipokiri kuwepo matatizo ya kuelewana kwa wasanii wa filamu hapa nchini, hali ambayo inarudisha nyuma maendeleo ya sanaa.

Waziri Nchimbi aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na timu ya soka ya Bongo Movies Club baada ya kumalizika kwa mchezo wa kirafiki kati yake na timu ya Bunge Sports Club uliochezwa kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma, ambapo Bunge Sports Club iliifunga Bongo Movies Club 2-1.

Jun 21, 2011

Filamu ya Maalim Seif yatikisaTamasha la filamu Zanzibar

 Maalim Seif Sharrif Hamad akiwa na Mtayarishaji Kiongozi wa Filamu yake, Javed wakati Filamu hiyo ikioneshwa katika ukumbi wa Ngome Kongwe Zanzibar

 
Maalim Seif Sharrif Hamad akiwahutubia wakazi wa Zanzibar waliofurika katika ukumbi wa Ngome Kongwe kushuhudia uzinduzi wa Filamu yake

Safari ya Makamu wa Rais wa Zanzibar kuelekea Ikulu iliyowekwa katika filamu na kampuni ya ZG na kuzinduliwa katika tamasha la 14 la Filamu visiwani Zanzibar juzi ilikuwa gumzo katika Ukumbi wa Ngome Kongwe na kuzoa umati wa watu kuishuhudia na ilizua upya hisia za kisiasa kiasi cha kumlazimu mhusika mkuu kutuliza hisia za watazamaji hao.

Filamu hiyo maalum inayoelezea maisha na harakati za maisha ya mwanasiasa huyo mkongwe ambaye ni makamu wa kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Maalim Seif Sharrif Hamad imepewa jina la A Journey to the State House na imetengenezwa na kampuni ya ZG inayojishughulisha na mambo ya filamu visiwani humo.

Pappa-Zi kufanya kongamano la filamu leo, Dar

 Rais wa TAFF, Simon Mwakifwamba

 Wasanii wa kikundi cha ABY cha Buguruni Malapa
wakiwa katika mazoezi ya sanaa

Kongamano la wadau na wasanii wa filamu Tanzania, litafanyika leo kwenye ukumbi wa Villa Park Resort jijini Dar es Salaam, pamoja na mambo mengine litazungumzia nafasi ya wasanii wa filamu nchini.

Kongamano hilo linafanyika chini ya kampuni ya Pappa-Zi ambayo ni kampuni mpya yenye madhumuni ya kuibua vipaji vya wasanii, kuendeleza na kusambaza kazi zao. Pappa-Zi imetangaza mikakati mipya ikiwa ni pamoja na kusimamia kazi za wasanii na kwa kuanzia, itakuwa jijini Dar es Salaam.

Waziri Nchimbi akiri wasanii hawaelewani

 Emmanuel Nchimbi

 Bongo Movie Club

Bunge la Tanzania mjini Dodoma

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Emmanuel Nchimbi, amekiri kuwa bado kuna matatizo makubwa ya kutoelewana kwa wasanii hapa nchini, hali ambayo inarudisha nyuma maendeleo ya sanaa.

Waziri Nchimbi aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na timu ya soka ya Bongo Movies Club mjini Dodoma baada ya kumalizika kwa mchezo wa kirafiki kati yake na timu ya Bunge Sports Club uliochezwa kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma, ambapo Bunge Sports Club iliifunga Bongo Movies Club magoli 2-1.

Nchimbi aliwataka wasanii kumaliza tofauti zao na kuwa na mshikamano na umoja ili waimarishe na kuboresha kazi zao za sanaa. Alisema (serikali) wataendelea kushirikiana na wasanii katika michezo ya kirafiki na masuala mbalimbali ya kijamii ili kujenga mahusiano mazuri kati yao (wabunge) na wasanii.

Jun 15, 2011

Tuhuma za kuwadhalilisha wasanii wa kike zinaichafua tasnia ya filamu

 Baadhi ya wasanii wa kike katika timu ya Bongo movie

 Mastaa wa filamu wanaounda timu ya Bongo Movie

 Rose Ndauka, mmoja wa wasanii wa filamu 
wa kike wenye mvuto wa aina yake

 Hatmann Mbilinyi, mwenyekiti wa Club

KATIKA karne hii ya 21 vyombo mbalimbali vya mawasiliano, kama vile, magazeti, simu, redio, kinasa sauti, runinga, video, mtandao na kadhalika, vinachangia sana katika kuifanya dunia yetu kuwa ndogo sana. Vinachangia pia katika kuuendeleza utandawazi, na katika usambazaji wa utamaduni wa Kimagharibi kwa nchi zetu.

Vyombo hivi vimekuwa vikitumika kwa ajili ya kujielimisha na kujiburudisha, na maendeleo ya vyombo hivi yanakua kila siku kutokana na kuvumbuliwa kwa teknolojia mpya na rahisi kutumia.

FILAMU ZA BONGO: Sumu mbaya iliyopandikizwa kuhusu sinema za Part 1 na 2

 Naomi Part 1

Naomi part 2

NAUHUSUDU sana mkoa wa Tanga, mkoa wanakotoka magwiji wa filamu waliothubutu kuandaa filamu miaka ya tisini japo mazingira yalikuwa magumu; ingawa filamu iliyowazindua wengi ni 'Girlfriend' (2002) chini ya uongozaji wa George Otieno “Tyson”, lakini ni filamu ya 'Shamba Kubwa' (1995) iliyotungwa na kuongozwa na Mwl. Kassim Al Siagi wa Tanga ndiyo iliyofungua milango ya filamu za kibiashara hapa nchini.

Kipindi kile teknolojia ilikuwa bado ndogo na vituo vya televisheni ndo kwanza vilikuwa vimeanza. Wakati huo kulikuwa na vituo vya ITV na CTN tu ambavyo hata hivyo vilirusha matangazo yake hapahapa jijini Dar es Salaam.

Jun 14, 2011

Tetesi: Ufuska na udharirishaji Bongo Movie Club

 Timu ya Bongo Movie Club ndani ya Mwanza

 Wasanii wa kike wa Bongo Movie Club

 Baadhi ya wadau wa Bongo Movie Club

Bongo Movie Club wanajiandaa kwenda Dodoma kwa ajili ya mechi yao na Wabunge hapo Ijumaa, lakini tayari kuna kashfa imeikumba club hiyo na viongozi wanajitahidi kuzima kashfa isijulikane kwenye vyombo vya habari kabla hawajacheza na wabunge.

Jana kutwa nzima na hata leo wana kikao cha kuweka mambo sawa hasa. Nimebahatika kuipata
meseji iliyotumwa na Msani mmoja wa kike kwenda kwa viongozi wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) akiwalalamikia, meseji yenyewe ni hii (sijaongeza neno ingawa majina ya wahusika nimeyahifadhi):

Ni msg yenu VIONGOZI kabla ya safari ya Dodoma; Kumekuwepo unyanyasaji mkubwa kwenye CLUB, ngono, majungu na ufisadi. msanii wa kike aitwaye (linatajwa jina) kagaragazwa sana na (jina la msanii wa kiume) walipokwenda Mwanza. (Jina la kiongozi mmoja wa club) kawagaragaza (linatajwa jina) na (linatajwa jina), na bado kuna wengine anawahitaji, tena kwa nguvu, nyie mmekaa kimya!


Huyo (msanii aliyemdharilisha mwenzake Mwanza) na (huyu alikuwa kiongozi wa TAFF enzi zile) wamegeuza CLUB sehemu ya kujipatia pesa kwa mapedeshee. ONYO hatukuja kugarazazwa tuheshimiwe la sivyo tutaripoti kwenye vyombo vya habari.

 
Mwisho wa kunukuu. Hapo kwenye maneno yenye RED nimebadili maneno yaliyoandikwa kwa sababu za kimaadili.
 
Inasikitisha sana kuona tabia kama hizi zikijitokeza kwa watu tunaoamini kuwa ni kioo cha jamii na waliopaswa kuwa mfano mzuri kwenye jamii yetu.

Jun 8, 2011

Steps wamepandikiza sumu mbaya kwa watazamaji wa filamu Tanzania

 Wasanii wanaoitwa Mastaa wa lebo ya Steps

Mkurugenzi wa kampuni ya Steps, Dilesh

HIVI karibuni nilikuwa nabadilishana mawazo na mdau muhimu sana katika tasnia ya filamu hapa nchini, Hamisi Kibari, ambaye pia ndiye mhariri wa gazeti hili. Nilivutiwa sana na kisa alichonisimulia kuhusu dada yake, Rehema Kibari (maarufu kama Mama Rashid), ambaye ni hakimu wa mahakama ya mwazo huko Kilwa Kivinje. Kisa hicho ndicho kimenifanya kuandika makala haya.

Dada huyo alimtembelea Kibari nyumbani kwake, Temeke jijini Dar es Salaam na kutaka kujua kama bado anajihusisha na masuala ya filamu. Kibari ambaye kwa mara ya mwisho alitoa filamu ya 'Mtoto wa RPC' mwaka 2007, akaona huo ni wakati mzuri wa kumuwekea dada yake filamu yake mpya ya Naomi (sinema ya mwisho kuchezwa na Tabia wa Kidedea) aliyomaliza kuihariri na inayotarajiwa kuingia sokoni wakati wowote kuanzia sasa, ili kupata maoni.

Waziri Mponda ataka filamu ziwe somo la Malaria

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Haji Mponda

Muongozaji wa Filamu ya Chumo, Jordan Riber (katikati) 
akitoa maelezo juu ya Filamu hiyo. Kushoto ni baba yake 
ambaye pia ni mtengenezaji wa filamu, John Riber.

Baadhi ya washiriki wa sinema hiyo

 Baadhi ya wadau waliofika kwenye uzinduzi wa filamu hiyo

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Haji Mponda amewataka wadau wa filamu na burudani nchini kutumia sanaa katika kuelimisha jamii kuhusu ugonjwa wa Malaria. Mponda amesema hayo baada ya uzinduzi wa filamu ya Chumo yenye dakika 45 inayoelimisha jamii kuhusu ugonjwa wa Malaria pamoja na kutoa suluhisho katika kupambana na ugonjwa huo.

Mponda alisema kuwa anatambua mchango wa sanaa katika kuelimisha jamii na kuongeza kuwa kupitia sanaa wanajamii wanaweza kuelimika kirahisi zaidi na kuepuka uwezekano wa kupata ugonjwa huo.

Jun 1, 2011

Tuhuma za Steps kuwagawa wasanii na utetezi dhaifu!

 Filamu ya White Chair, moja ya sinema zilizokumbwa na kadhia ya kulazimishwa kuingiza sura zinazodaiwa kuuza

 Msanii Issa Mussa maaruf kama Claude

 Mtengeneza filamu maaruf, John Riber

SIKU zote naamini kuwa penye ukweli uongo hujitenga. Jumamosi iliyopita, katika kipindi cha Baragumu kinachorushwa asubuhi kwenye moja ya vituo vyetu vya televisheni kulikuwa na mada inayozungumzia changamoto zinazoigusa tasnia ya filamu Tanzania, ambapo kampuni ya usambazaji wa filamu ya Steps Entertainment ilimtuma mwakilishi wake, anayejiita Kambarage, kujibu baadhi ya tuhuma zinazoikabili kampuni hiyo.

Kwa kweli sikutegemea kwa kampuni kubwa inayoaminika kuwa na watu makini kama Steps Entertainment kuwakilishwa na msemaji wa aina ile aliyeishia kujisifia kwa kusafiri kwenda Kenya, Burundi, Rwanda na Kongo, lakini akionekana kutojua mambo mengi kwa jinsi alivyokuwa akibabaika kujieleza, japo mwendeshaji wa kipindi, Fred Mwanjala alionekana kumuuliza maswali ya kumbeba.