Jun 21, 2011

Waziri Nchimbi akiri wasanii hawaelewani

 Emmanuel Nchimbi

 Bongo Movie Club

Bunge la Tanzania mjini Dodoma

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Emmanuel Nchimbi, amekiri kuwa bado kuna matatizo makubwa ya kutoelewana kwa wasanii hapa nchini, hali ambayo inarudisha nyuma maendeleo ya sanaa.

Waziri Nchimbi aliyasema hayo alipokuwa akizungumza na timu ya soka ya Bongo Movies Club mjini Dodoma baada ya kumalizika kwa mchezo wa kirafiki kati yake na timu ya Bunge Sports Club uliochezwa kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma, ambapo Bunge Sports Club iliifunga Bongo Movies Club magoli 2-1.

Nchimbi aliwataka wasanii kumaliza tofauti zao na kuwa na mshikamano na umoja ili waimarishe na kuboresha kazi zao za sanaa. Alisema (serikali) wataendelea kushirikiana na wasanii katika michezo ya kirafiki na masuala mbalimbali ya kijamii ili kujenga mahusiano mazuri kati yao (wabunge) na wasanii.

No comments: