Sep 20, 2011

IJUE BODI YA FILAMU TANZANIA

 Nembo ya Tanzania

 Rose S. Sayore, Mwenyekiti wa Bodi ya Filamu

Merybeatrix Mugishagwe, Mjumbe wa Bodi

HISTORIA YA BODI YA UKAGUZI WA FILAMU TANZANIA

Historia ya bodi ya Filamu nchini Tanzania inaanzia kipindi cha utawala wa kikoloni ambapo mwaka 1930 Sheria ya Picha za Sinema ilitungwa na kuanza kutumika. Mnamo mwaka 1974 Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania lilitunga namba 4 Sheria ya Filamu na Michezo ya Kuigiza na mnamo mwaka 1976 na sheria hiyo ilisainiwa na rais wa wakati huo Mwalimu Julius K. Nyerere.Sheria ambayo ina tumiaka mpaka sasa. Majukumu ya Bodi ni kulinda Utamaduni kwa kuhakikisha kuwa sanaa ya filamu na michezo ya kuigiza inazingatia maadili ya Taifa.
Jukumu lake kubwa ni kukagua filamu na kanda za video,vikundi vya sanaa za maonyesho na kutoa ushauri kwa kuzingatia maadili.

Mwaka 2011 Kanuni za Sheria ya Filamu na Michezo ya Kuigiza namba 4 ya mwaka 1976 zilikamilika na kuanza kutumika. Kanuni hizo zimetangazwa katika gazzeti ya Serikali namba 156/ 2011.Kanuni hizi zimeiongezea Sheria ya Filamu uwezo wa utekelezaji.

Filamu ni Picha yoyote Jongevu. Picha Jongevu ni mpangilio wa picha ya kitu au vitu vinavyoonekana na vilivyorekodiwa katika kifaa chaochote cha kwa mfumo wa digitali,seluloid, au kwa namna yoyote ambayo picha hiyo inaweza kujongea na inajumuishapicha zilizoko katika mfumo wa filamu, video,katuni na picha zozote zinazofanana na hizo

Muundo wa bodi ya filamu umegawanyika wa wajumbe wa bodi za wilaya, mikoa na bodi kuu ya Taifa. Kwa sasa bodi kuu ya kitaifa ina wajumbe saba (7) ambao huchukua madaraka kwa kipindi cha miaka mitatu (3) na wanaweza kuteuliwa tena kwa mujibu wa kanuni zinazoongoza bodi.
Katika wajumbe saba wa filamu, Katibu Mtendaji wa Bodi ya Ukaguzi wa Filamu, ndiye katibu wa bodi ya wajumbe wa Bodi ya Ukaguzi wa Filamu.

Wajumbe wa sasa wa bodi ya Bodi ya Ukaguzi wa Filamu Tanzania ni kama ifuatavyo:
1.Bi. Rose S. Sayore (Mwenyekiti)
2.Bi. Fisso (Katibu)
3.Bi. Merybeatrix Mugishagwe (Mjumbe)
4. Bw. Barnabas Mwakalukwa (Mjumbe)
5. Bw. Sylvester J.A. Sengerema (Mjumbe)
6. Bw. Bechimana Gama (Mjumbe)
7. Bw. Kassim Twaribu (Mjumbe)

WASIFU MFUPI WA WAJUMBE WA BODI YA BODI YA UKAGUZI WA FILAMU TANZANIA
Ufuatao ni wasifu mfupi wa Wajumbe wa Bodi ya Bodi ya Ukaguzi wa Filamu Tanzania:

1. Bi. Rose S. Sayore (Mwenyekiti)
Huyu ndiye Mwenyekiti wa Wajumbe wa Bodi ya Bodi ya Ukaguzi wa Filamu Tanzania. Kitaaluma Bi. Rose S. Sayore, kitaaluma ana BA. General Theatre Arts (UDSM), pia ana diploma ya Upigaji picha (Diploma of Photography Art and Motion Picture) ya Toronto Canada, pia ana Bachelor of Applied Arts (Photographic Art) ya Toronto. Amekuwa ni mjumbe ya Bodi ya Taifa ya Ukaguzi wa Filamu tangu mwaka 1994. Pia ni Mkuu wa kitengo cha Kuhariri Picha za Filamu katika Chuo cha Audio Visual cha Dar es Salaam. Nyadhifa nyingine zinazoshikiliwa na Bi. Rose ni Katibu Msaidizi wa Baraza la Sanaa la Taifa.

2. Mrs. Joyce Fisso (Katibu)
Bi. Fisso ni Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania, na kwa wadhifa wake ndiye katibu wa Bodi ya Wajumbe wa Bodi ya Ukaguzi wa Filamu Tanzania. Kitaaluma Bi. Fisso ana Shahada ya pili ya Sanaa ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Pia ana Shahada ya kwanza ya BA (Hon.) Theatre Arts ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Nimtaalamu wa Kuandika miswada ya filamu, kuongoza na kucheza filamu.

3. Merybeatrix Mugishagwe (Mjumbe)
Huyu ni moja ya wajumbe wa Bodi ya Ukaguzi wa Filamu, ambaye kitaaluma ana Shahada ya  Mass Communication, na Shahada ya pili ya Mass Communication ya Munich, Ujerumani. Kwa sasa anashikiliawWadhifa wa Mtendaji Mkuu wa Abantu Vision. Ambaye katika Bodi hii ni mwakilishi wa Watunzi na Waendeshaji wa Filamu.

4. Barnabas Mwakalukwa (Mjumbe)
Huyu pia ni moja ya wajumbe wa Bodi ya Ukaguzi wa Filamu akimwakilisha Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania. Kitaaluma ana Shahada ya kwanza ya Usimamizi wa Biashara (BBA).

5. Sylvester J.A. Sengerema (Mjumbe)
Bw. Sylvester J.A. Sengerema kitaaluma ni Mwanasheria akiwa na Shahada ya Kwanza ya Sheria ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Pia ana Diploma ya Mass Communication, Maendeleo Vijijini na Mipango.

6. Bechimana Gama (Mjumbe)
Ni mjumbe wa Bodi ambaye pia ni Ofisa mkuu katika Ofisi ya Ukaguzi wa Filamu (Senior Officer of Film Censure Office). Kitaaluma ana Diploma ya Theatre Arts.

7. Kassim Twaribu (Mjumbe)
Bw. Kassim Twaribu ni miongoni mwa wajumbe wa Bodi akiwakilisha kundi la Chama la Wasanii Tanzania. Alionekana sana katika michezo ya televisheni iliyorushwa katika kituo cha ITV katika miaka ya 1990 na kuendelea. Kitaaluma ana Diploma ya Elimu.

Sekretarieti
Sekretariati ina wajumbe saba (8), ikimjumuisha Katibu Mtendaji wa Bodi, Bi Joyce Fissoo,
Bi. Tabu Magembe ambaye ni Principle Cultural Officer. Bi. Tabu Magembe katika Bodi ya Ukaguzi wa Filamu anashikilia ofisi ya Mkaguzi wa Filamu na Kumbi za Maonyesho ya Sinema.
Makarage S. Nkinda: Huyu pia ni Ofisa wa Utamaduni. Kitaaluma ana shahada ya pili ya Maendeo Vijijini na Shahada ya kwanza ya Theatre Arts. Ana uzoefu katika kucheza na kuongoza filamu.
Beatrice K. Sumari: Bi Beatrice katika sekretariat ni Mkaguzi wa Filamu na huhusika na utoaji wa vibali vya kutengeneza Filamu. Kitaaluma ana Shahada ya Kwanza Anthropologia.
Romanus W. Tairo: Bw. Tairo katika sekretariat anashikilia ofisi ya Usimamizi wa utoaji wa leseni mbalimbali zitolewazo na bodi, kutunza kumbukumbu za wasambazaji. Kitaaluma Bw. Tairo ana Shahada ya kwanza ya Philosophia.
Mwaswala Jonas: Huyu ni Mtunza Stoo ya Bodi ya Ukaguzi wa Filamu Tanzania.
Fatuma Kipyate: Bi Kipyate ni msaidizi wa Mtendaji Mkuu.
Jackson Ntiro: Ni dereva
Sekretariat pia inapata wataalamu mbalimbali kutoka katika Wizarani, idara ya Utamaduni, Idara za TEKNOHAM, Sheria na Fedha,.

Kamati ya Kimwingiliano Kiwizara (Inter Ministerial Committee)
1. Waziri wa Habari Vijana Utamaduni, na Michezo
2. Katibu Mtendaji – Bodi ya Ukaguzi wa Filamu Tanzania
3. Wakakilishi kutoka:
1. Idara ya Utamaduni
2. Idara ya Habari
3. Wizara ya Maliasaili na Utalii
4. Idara ya Uhamiaji
5. Mamlaka ya Mapato Tanzania
6. Polisi, Ikulu, na Mambo ya Nje.

Kwa mujibu wa Kifungu cha 28 cha Sheria ya Filamu na Michezo ya Kuigiza ya 1976, Katibu Mtendaji wa Bodi ya Ukaguzi wa Filamu na Michezo ya Kuigiza atateuliwa na Maziri mwenye dhamana.

Kazi za Bodi:
Kwa mujibu wa Sheria Na. 4 ya Filamu na Michezo ya Kuigiza ya mwaka 1976, bodi ina kazi zifuatazo:
 1. Kukagua filamu zote na kutoa ruhusa ya kuonyeshwa hadharani;
 2. Kutoa vibali vya utengenezaji wa filamu kwa watengenezaji kutoka nje ya nchi  na kusimamia utengenezaji wa Filamu zote nchini
 3. Kukubali/kutokukubali kutoa leseni/kibali kwaajili ya kufanya shughuli za filamu au michezo ya kuigiza nchini;
 4. Kukagua na kutoa Leseni za majumba ya sinema nchini;
 5. Kupitisha miswada na kuratibu maonyesho ya Michezo ya kuigiza;
 6. Kuratibu na kusimamia Bodi za Mikoa na Wilaya
 7. Kusimamia na kuratibu utendaji wa asasi zinazojishughulisha na masuala ya filamu Nchini ( vyama, mashirikisho, asasi n.k)
 8. Kutoa/kutotoa ruhusa ya matangazo ya filamu
 9. Kusimamia na kuratibu utekelezaji wa Sheria ya Filamu na Kanuni zake.
 10. Masharti mengine kwa mujibu wa sheria Na. 4 ya mwaka 1976 ya Bodi ya Filamu na kanuni zake ;

Hatua za Utoaji Vibali na Leseni
Mwombaji wa vibali au leseni kwaajili ya kufanya shughuli za filamu na michezo ya kuigiza nchini anapaswa kufuata taratibu zifuatazo:
 1. Kuandika barua ya maombi ya kutengeneza filamu;
 2. Kujaza fomu za maombi ya leseni/kibali;
 3. Kuwasilisha miswada na kazi zilizokwishazalishwa kwa ukaguzi mfano: VHC, DVD, CD nk;
 4. Kulipia ada.

Taratibu nyingine ili kuweza kupata vuhusa ya kufanya shughuli za filamu nchini:
 • Kwa wazalishaji kutoka nje ya Tanzania
1. Mwomba lazima ajaze fomu ya maombi ya uzalishaji ambayo lazima isainiwe na Ubalozi wa Tanzania katika inchi anayotoka; Pamoja na taarifa za timu yake yote ya uzalishaji;
2. Mwombaji ataleta picha aina ya passport size;
3. Mwombaji ataambatanisha kivuli cha hati yake ya kusafiria
4. Mwombaji atawasilisha nakala ya mswada wa filamu inayotarajiwa kutengenezwa;
5. Kulipia ada:
Ø Huduma ya Haraka (Fast track) $3000
Ø Huduma ya Kawaida $1000

 • Kwa Wazalishaji Wazawa
1. Mwombaji atajaza fomu ya maombi ya uzalishaji, huku akizingatia kutoa taarifa za wasanii watakaocheza, gharama, na idadi ya nakala zitakazozalishwa;
2. Kuleta kwa bodi nakala ya zao la filamu ili likaguiliwe na kupewa daraja na bodi.

Ukaguzi wa Filamu
Kwa mujibu wa Sheria Na. 4 ya mwaka 1976 ya Filamu na Michezo ya Kuigiza; filamu zote za ndani na nje zinapaswa kukaguliwa na kupewa madaraja ya hapa nchini kuzingatia tamaduni, mila na maadili ya Kitanzania.

Kwa filamu za ndani, mwazalishaji wanapaswa kuleta nakala ya zao la filamu kwa ukaguzi kisha kupata/kutopata baraka za bodi kuweza kuzalisha na kusambaza filamu hizo. Tofauti na utaratibu huu, hakuna zao la filamu linalopaswa kusambazwa sokoni kabla ya kuonekana kwa Bodi ya Filamu na Michezo ya Kuigiza.

Gharama wa wazalishaji Wazawa:
Kwa mujibu wa kanuni ya Bodi ya Filamu na Michezo ya Kuigiza, wazalishaji wanapaswa kulipa ada kama ifuatavyo:
 1. Huduma ya Haraka (Fast Track) TSH. 1,000,000/-
 2. Huduma ya Kawaida TSH. 500,000/-

Kuanzia July 2011 kanuni ya Filamu inaagiza gharama za ukaguzi wa filamu utafanyika kwa dakika kama ifuatavyo:
 1. Mazao ya filamu yatakayozalishwa na wazawa itagharimu TSH. 1,000 kwa dakika
 2. Mazao ya filamu yatakayozalishwa na wasio wazawa yatagharimu $5 kwa dakika

Taratibu za Utoaji wa Leseni za Kumbi/ Majumba ya Sinema
Waombaji wa undeshaaji wa shughuli za kuonyesha sinema katika kumbi/majumba ya sinema wanapaswa kufuata taratibu zifuatazo:
 1. Kuandika barua ya maombi ya kibali ya uendeshaji wa kumbi/jumba la sinema
 2. Bodi kuu na bodi za wilaya zitakagua ukumbi/jumba lililoombewa kibali kama linakidhi viwango vya kiafya, kiusalama na kimiundombinu kwa mujibu wa taratibu na kanuni;
 3. Bodi itatoa daraja kwa kila ukumbu utakao kidhi viwango
 4. Bodi itatoa leseni ya uendeshaji kumbi na majumba ya sinema

Leseni za Wasambazaji
Wasambazaji wote wa filamu wanapaswa kukaguliwa, kupewa vibali, leseni na ruhusa ya kufanya au kuendesha shughuli za usambazaji wa mazao ya filamu hapa nchini. Wazambazaji watakao kidhi matakwa watapewa leseni za uendeshaji wa shughuli za usambazaji wa filamu na Bodi ya filamu. Wasambazaji na wafanyakazi wote wa usambazaji wanapaswa kupewa kitambulisho na Bodi Kuu ya Filamu, Bodi za Wilaya

Wanaopaswa kukaguliwa, kupewa vibali, leseni na ruhusa za kufanya au kuendesha shughuli za filamu nchini ni hawa wafuatao:
 1. Watunzi wa michezo ya kuigiza ya runinga ;
 2. Waandishi wa miswada ya michezo ya kuigiza na filamu;
 3. Waandaji wa matangazo, maigizo na matangazo mengine;
 4. Wapiga picha za sinema kwa vifaa vya kielekroniki;
 5. Waongozazi wa utengenezaji wa filamu;
 6. Wasambazaji wa filamu;
 7. Waonyeshaji wa filamu;
 8. Wenye majumba/kumbi za sinema, sehemu za wazi na vyombo vya usafiri nk.
 9. Asasi /vyama vinavyojishughulisha na masuala ya filamu nchini.
   
  Madaraja ya Filamu Tanzania
  Daraja Maelezo
  U Filamu katika daraja hili inafaa kutazamwa
  na watu wa daraja zote
  A13 Filamu katika daraja hili inafaa kutazamwa
  na watoto walio na umri wa miaka 13
  wanapokuwa na watu wazima
  A16 Filamu katika daraja hili inafaa kutazamwa
  na watoto walio na umri wa miaka 16
  wanapokuwa na watu wazima
  A18 Filamu katika daraja hili inafaa kutazamwa
  na walio na umri wa miaka 18
  R Imekataliwa (rejected)
  X Filamu hizi haziruhusiwa kabisa nchini
  Tanzania

No comments: