Jun 20, 2012

Dk. Mgimwa, hili la stampu za TRA na kuirasimisha tasnia ya filamu ni sawa, lakini…

 Waziri wa Fedha, Dk. William Mgimwa

“MHESHIMIWA Spika, napendekeza kufanya marekebisho katika Sheria ya Ushuru wa Bidhaa, SURA 147 kama ifuatavyo:-

“Mheshimiwa Spika, kumekuwa na kilio cha muda mrefu cha wasanii kudurufiwa kazi zao za sanaa na kukosa maslahi kwa kazi wanazofanya. Ili kutatua tatizo hili, Serikali kupitia Mamlaka ya Mapato itaanza kurasimisha biashara ya bidhaa za muziki na filamu kwa nia ya kuhakikisha kwamba uasili wake unatambulika na hivyo kuzuia vitendo vya kudurufu kazi za sanaa (piracy of artists work) hali ambayo inadumaza ukuaji wa sanaa na vipaji hapa nchini.

Gaba Arts Centre na Basata watoa somo kwa wasanii wa filamu


Mkurugenzi wa asasi ya Gaba Arts Centre, James Gayo, akisisitiza jambo wakati akitoa mafunzo kwa wasanii wa filamu juu ya Stadi za Uandishi wa Miswada ya Sinema (Script) kwenye Jukwaa la Sanaa linalofanyika kila wiki makao ya Baraza la Sanaa la Taifa (Basata)

Asasi ya Gaba Arts Centre na Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) Jumatatu ya wiki hii 18, Juni 2012, saa 4 kamili kwenye jukwaa la sanaa waliendesha semina fupi kwa Wadau/wasanii wa filamu ili kuwajengea weledi katika eneo la uandishi bora wa miswada ya sinema (scriptwriting).

Warsha hiyo ya saa mbili ilihusu zaidi Stadi za uandishi wa miswada ya Sinema (Script writing skills), baadhi ya mambo yaliyojadiliwa ni:

Jun 17, 2012

Tamasha la filamu la wazi kufanyika Tanga Juni 2012


Tamasha kubwa la filamu la wazi linatarajiwa kuanza tarehe 30 mwezi huu, tamasha hilo linajulikana kwa jina la Grand Malt Tanzania Open Film Festival (TOFF) na litafanyika jijini Tanga kwa mara ya nne katika viwanja vya Tangamano, ambapo litadumu kwa muda wa siku saba, na kwa kila siku zitaonyeshwa filamu tatu.

Mkurugenzi wa kampuni ya Sofia Production ya Jijini Dar es Salaam, Mussa Kisoki, amesema kuwa kila kitu kimekamilika kwa ajili ya tamasha hilo ambalo linafanyika kwa mwaka wa nne toka kuasisiwa kwake.

Jun 6, 2012

Filamu za Nigeria zinapotumika kama kipimo cha filamu zetu!


Desmond Elliot, muigizaji wa Nollywood ambaye alikuwa 
akiigwa na Steven Kanumba katika uigizaji wake

Marehemu Steven Kanumba

SEKTA ya filamu Tanzania kwa sasa inajulikana duniani licha ya matatizo yake, licha ya mtayarishaji wa filamu wa Tanzania kuendelea kuishi maisha ya chini yasiyo tofauti na mtu mwingine wa kawaida! Sekta ya filamu Tanzania inakua, lakini hali halisi ya soko la filamu nchini inabana sana uwezekano wa kuibuka kwa wasanii, watayarishaji au waongozaji wapya...

Sidhani kama kuna mtu atakayebisha kuwa filamu za kibongo ‘hazitesi’ katika ukanda wa Afrika Mashariki na maeneo ya Maziwa Makuu. Filamu hizi zimesaidia kwa kiwango fulani kuitangaza nchi hii, kuwatangaza wasanii wa nchi hii, lakini vipi kuhusu maisha ya wasanii hawa? Je, wanapata stahili yao na wanaishi kwa kutegemea filamu pekee?

Jun 4, 2012

Wasanii Bongo Movie na madai ya ukahaba, kupiga picha chafu
Ni muda mrefu imekuwa ikisemwa kuwa wasanii wanaoendesha maisha yao kwa ‘kuuza nyago’ kwenye filamu za Kibongo ni watu wanaojiuza, kufanya ufuska na kupiga picha za utupu, ambapo imeshawahi kutolea orodha ndefu ya wasanii hao, huku wengine wakiondoka nchini na kwenda kufanya ufuska huo nje ya Tanzania.


Madai ya kufanya ufuska yaliwahi kuthibitishwa na msanii wa filamu Bongo, Coletha Raymond ‘Koleta" aliyesema kuwa “Kiukweli sanaa inatufanya wasanii wa kike tuingie kwenye vitendo vya umalaya. Sanaa ya Bongo ni vigumu sana kutoka, hailipi kabisa... yaani inatakiwa mtu ufanye kazi nyingine tofauti ndiyo uweze kufanikiwa. Wasanii unaowaona wamefanikiwa si kwa filamu pekee, wana mambo mengine,” alisema na kuongeza: