Feb 24, 2012

Tutumie nafasi za kujikosoa kuboresha kazi zetu.

Mmoja wa wasanii wenye mafanikio kisanii nchini Tanzania,
Yvonne Cherryl maarufu kwa jina la Monalisa

HIVI karibuni nilikuwa katika kikao cha wadau saba wa filamu waliopendekezwa kuunda kamati maalum itakayokuwa na lengo kuu la kupitia na kutoa maoni katika filamu zetu, ili kuziboresha na hatimaye kuongeza ufanisi katika uzalishaji wa filamu kwenye tasnia hii nchini. Kamati hiyo ya watu saba ilipendekezwa na wadau mbalimbali wa filamu kwa kupiga kura kupitia mtandao wa kijamii wa facebook/ Tanzania Film Critics Association.

Ukosoaji wa filamu duniani ni uchambuzi na utathmini wa filamu, iwe kwa mtu mmoja mmoja au kwa pamoja. Kwa ujumla, kazi hii ya ukosoaji wa filamu inaweza kugawanywa katika makundi mbalimbali kama vile mapitio ya filamu yanayofanywa na waandishi wa habari ambayo huonekana mara kwa mara katika magazeti,

Feb 17, 2012

The making of the Fasta Fasta short film
Hivi ndivyo filamu fupi ya Fasta fasta ilivyoandaliwa...

Mambo ni Fasta Fasta katika Movie ya Fasta FastaFasta Fasta! Filamu fupi (short film) iliyotengenezwa na vijana wa Kitanzania kama sehemu ya mafunzo ya wiki mbili yaliyoendeshwa mwaka 2010 na Matthias Luthardt (Muongozaji maarufu wa Ujerumani) na Frédéric Théry (Mtaalamu wa Sauti kutoka Ufaransa).

Mafunzo haya yaliandaliwa na Taasisi ya Kijerumani ya Goethe-Institut kwa kushirikiana na Taasisi ya Ufaransa ya Alliance Francaise na kudhaminiwa na Elysée-Fonds na Tamasha la Filamu la Nchi za Ulaya (European Film Festival). Filamu hii ipo katika Kiswahili na ina subtitle za Kiingereza.

Walioshiriki kuiandaa ni:
Bishop Hiluka, Christina Pande, Deepesh Shapriya, Elie Chansa, Emmanuel Munisi, godfrey Semwaiko, Nassos Chatzopoulos, Octivan Francis, Peter Mbwago, Smith Kimaro, Theresia Makene na Nina Mnaya.

Ni kweli tumeshindwa kukomesha wizi wa filamu?

DVD feki zikiwa tayari kwa kuuzwa

Hakuna ubishi kuwa nguvu zaidi zinahitajika katika kufanikisha mapambano ya kuwakomboa wasanii, watengenezaji na wasambazaji wa kazi za sanaa ili wapate malipo/mapato stahiki kutokana na kazi zao. Nashangaa kuwa Chama cha Hakimiliki na Hakishiriki (Cosota) kimeonekana kulala usingizi, badala ya kuchukua hatua.Sehemu kubwa ya umma – wakiwemo wasanii wenyewe - haijui chochote kuhusu Sheria ya Hakimiliki na Hakishiriki, hata Cosota bado haichukui hatua madhubuti za kuendesha kampeni kamambe nchi nzima ili kuuelimisha umma pamoja na wasanii kuhusu Sheria ya Hakimiliki na Hakishiriki.

Feb 15, 2012

RIP Mwandishi Faraji H. Katalambula Mtunzi wa "Simu ya Kifo"

Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo Muhammad Seif Khatib akimpongeza mtunzi wa riwaya Faraji H.H. Katalambula kwa umahiri wake kwenye fasihi. Hii ilikuwa wakati wa uzinduzi wa filamu ya Simu ya Kifo iliyotokana na riwaya yake.


Mwandishi Faraji H. H. Katalambula hayupo tena duniani. Amefariki jioni ya Jumanne wiki iliyopita katika Hospitali ya Taifa Muhimbili. Mzee Katalambula alikuwa mmoja wa watunzi mahiri wa vitabu kupata kutokea nchini mwetu, atakumbukwa zaidi kwa utunzi wake wa kitabu kilichosomwa sana cha “Simu ya Kifo” ambacho baadaye kilitengenezewa filamu iliyoongozwa na gwiji mwingine wa riwaya, ambaye pia hatunaye, Hammie Rajab.

Taarifa za msiba zilisambazwa na mdogo wa marehemu Gideon Katalambula. Msiba ulikuwa nyumbani kwa Marehemu, Mbagala Majimatitu. Mzee Katalambula alikuwa rafiki yangu, na nimewahi kuandika makala kuhusiana na mazungumzo yetu, kwani alifikiria sana kutengeneza filamu kwa kutumia hadithi zake.