Aug 29, 2012

Kama inataka kuboresha filamu, Serikali ituondolee kwanza huu mkanganyiko

Katibu Mtendaji wa Bodi ya Ukaguzi wa Filamu, Joyce Fisoo

Katibu Mtendaji wa Basata, Ghonche Materego

WIKI iliyopita niliandika makala kuhusu umoja mpya wa wasanii, watayarishaji na wadau wa filamu ulioanzishwa hivi karibuni kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya Leaders Club na kuweka historia mpya kwa kuifanya tasnia ya filamu kuzaliwa upya kwa kuwa na kundi moja lenye nguvu na uhamasishaji katika kutafuta maendeleo na pia kupambana na uharamia ambao umekuwa ukiwarudisha nyuma wasanii na kuwanufaisha wachache bila ya wao kutokwa jasho hata kidogo.

Aug 22, 2012

Umoja huu mpya wa wasanii usiishie kwenye kupambana na uharamia tu, uende mbali zaidi

TAFF mpya

KAMA tukiamua kuangalia sekta iliyosheheni utajiri mkubwa lakini inayoongoza kwa wadau wake kuwa fukara (imefukarishwa makusudi na watu wachache) na inazongwa na matatizo makubwa, basi sekta ya filamu itashika namba moja. Tathmini nyingi zilizofanyika na zinazoendelea kufanyika zinabaini kuwa chanzo kikuu cha matatizo haya ni kutoeleweka kwa dhana nzima ya biashara ya burudani hususan filamu, kutothaminiwa kwa filamu, kutokupewa kipaumbele na watunga sera katika mipango ya maendeleo ya nchi yetu, na mgawanyiko miongoni mwa wadau wa tasnia hii.