Dec 19, 2012

Urasimishaji sekta ya burudani: TRA inapojitwisha zigo isilolifanyia utafiti kwa lengo la kuongeza pato!


Wasanii wakifuatilia semina ya TRA kwenye ukumbi wa maonesho wa Makumbusho ya Taifa, Jumanne wiki hii

Pia nilikuwepo kwenye semina hiyo, hapa nipo na mdau

NIMEKUWA nikisisitiza kuwa hakuna 'excuse' yoyote kwa wasanii katika kukuza pato lao, kuondokana na umaskini na hata kushindana kimataifa kama hawataingizwa kwenye mfumo rasmi ambao utawafanya watambulike ndani na nje ya nchi ili kujenga mazingira ya wao kuweza kukopesheka, kupata fursa za kikazi na kukuza kazi wanazozifanya. Katika mataifa mengine wasanii wako rasmi na wameweza kuvuma na kupaa kiuchumi.

Lakini pia nimekuwa nikitoa wito kwa serikali kutumia fursa ya kuirasimisha tasnia ya burudani hususani filamu kwa kutuanzishia chombo cha kusaidia maendeleo ya miradi kama sehemu muhimu ya kuifanya sekta hii ifikie tunapopataka, na ni msingi muhimu ambapo mkakati wowote wa utengenezaji wa filamu unapaswa kujengwa.

Dec 12, 2012

Kurasmisha sekta ya filamu/muziki sawa lakini kwa hili la stempu tunakurupuka


Afisa Utafiti Mwandamizi wa TRA, Ephraim Mdee, akielezea
kuhusu stempu maalum zitakazoanza kutumia mwakani

BADO naikumbuka hotuba ya Waziri wa Fedha na Uchumi, William Mgimwa, aliyoitoa katika kikao cha bunge la bajeti kwa mwaka 2012/13, pale aliposema: “Mheshimiwa Spika, napendekeza kufanya marekebisho katika Sheria ya Ushuru wa Bidhaa, SURA 147 kama ifuatavyo:-
“Mheshimiwa Spika, kumekuwa na kilio cha muda mrefu cha wasanii kudurufiwa kazi zao za sanaa na kukosa maslahi kwa kazi wanazofanya. Ili kutatua tatizo hili, Serikali kupitia Mamlaka ya Mapato itaanza kurasimisha biashara ya bidhaa za muziki na filamu kwa nia ya kuhakikisha kwamba uasili wake unatambulika na hivyo kuzuia vitendo vya kudurufu kazi za sanaa hali ambayo inadumaza ukuaji wa sanaa na vipaji hapa nchini.