Apr 25, 2012

Ni nini kitatusaidia kufikia mafanikio ya soko la filamu?


Ukurasa wa facebook unaweza kutumika kutangaza sinema

Pia unaweza kutumia ukurasa katika mtandao wa Youtube

TASNIA ya filamu nchini ni sawa na mtoto yatima lakini hali hii isiwe sababu ya kutufanya kulipua kazi zetu, bali tunapaswa kuangalia namna iliyo nzuri itakayotuwezesha kuboresha kazi zetu na kufanikiwa katika soko la ndani na hata nje ya Tanzania. Nimewahi kudokeza katika siku za nyuma kuhusu vigezo muhimu viwili vinavyoweza kutuongoza katika dhana nzima ya mafanikio hasa tunapolifikiria soko la filamu: Maudhui/Mahitaji ya Watazamaji na Jukwaa la Uwasilishaji.

Tunapaswa kwanza kuwaelewa watazamaji wetu kabla ya kufanya chochote, kwani ni hatua muhimu sana katika mchakato wa biashara ya filamu.

Apr 23, 2012

Kifo cha Kanumba: Ray, Mange kortini...Vincent Kigosi 'Ray'

Mange Kimambi

Elizabeth Michael 'Lulu'

Jinsi kifo cha muigizaji staa wa Bongo Movies, Steven Kanumba kilivyotokea, kilikuwa lazima kiibue mshindo mkubwa na ‘apdeti’ ni kwamba msanii mwingine wa Bongo Movie, Vincent Kigosi maarufu kwa jina la ‘Ray’ atasimama kortini na mwanamke kiroporopo, Mange Kimambi.

Ray, amejiapiza kuwa lazima amfikishe Mange mahakamani kwa sababu ya kumzulia tuhuma kwamba yeye ndiye aliyehusika na kifo cha Kanumba.

Apr 18, 2012

Kwa wenzetu hutengeneza pesa hata wanapokuwa kaburini, sisi ni maumivu

Robert Nesta Marley (Bob Marley)

Steven Charles Kanumba

SEKTA ya filamu nchini ni sekta kubwa sana, yenye nguvu kubwa na ushawishi mkubwa mno, lakini ndiyo sekta isiyopewa kipaumbele kama sekta muhimu inayoweza kuchangia pato kubwa kwa maendeleo na ukuaji wa uchumi wa taifa letu. Sekta hii imefukarishwa makusudi na watu wachache, ndiyo maana wajasiriamali wa soko la filamu wanafanya kazi kwa nguvu zote lakini hawapati kile wanachostahili.

Ukitaka kujua kuwa sekta hii imefukarishwa hebu mtazame mtayarishaji wa sinema za Tanzania (achilia mbali msanii), hana kabisa hadhi ya kuitwa mtayarishaji wa sinema, hana kipato wala ushawishi ukilinganisha na sekta nyingine, wakati sinema ndiyo nyenzo kuu ya kupashana habari na kuelimishana.

Utajiri wa Steven Kanumba

* Ni magari matatu, viwanja kadhaa
* Mazishi yagharinu mil.52/-
Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiongea na mwenyekiti 
wa kamati ya mazishi Gabriel Mtitu

Moja ya gari tatu zilizoachwa na marehemu Kanumba

Kamati Kuu ya Mazishi ya aliyekuwa msanii mashuhuri wa filamu nchini, marehemu Steven Kanumba, imedai msanii huyo amefariki dunia akiwa maskini, kinyume kabisa cha umaarufu mkubwa aliokuwa nao wakati wa uhai wake.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Mtitu Gabriel, alisema hayo wakati akitoa ufafanuzi kuhusu makusanyo na matumizi ya fedha zilizotumika katika maombolezo, kuaga na mazishi ya Kanumba, aliyefariki dunia Aprili 7, mwaka huu na kuzikwa Aprili 10, mwaka huu.

Mbali na Mtitu kutoa ufafanuzi kuhusiana na fedha zilizokusanywa pamoja na matumizi yake, alikanusha taarifa za uvumi kuwa msanii huyo ameacha mali zenye thamani ya Sh. milioni 700.

Apr 17, 2012

Rambirambi za msiba wa Kanumba zachachuliwa

Steven Charles Kanumba, enzi za uhai wake

Waigizaji wa filamu nchini, Mahsen Awadh (Cheni) 
na Issa Mussa (Claude) kwenye msiba wa Kanumba.
Claude ndiye aliyekuwa mwekahazina wa kamati
ya mazishi ya Kanumba

Wananchi wakimuaga Kanumba kwenye viwanja 
vya Leaders Club

Uongozi wa Bongo Movie uliohusika na uratibu wa shughuli za mazishi ikiwemo michango katika msiba wa msanii Steven Kanumba, umeingia kwenye kashfa nzito. Kwa mujibu wa chanzo cha uhakika kutoka ndani ya familia ya Kanumba, kamati hiyo imedaiwa kufanya uchakachuaji wa michango hiyo inayokadiriwa kuwa mamilioni ya fedha, achilia mbali vitu kadhaa, yakiwemo magunia 32 ya mchele.

Inasemekana kuwa, dalili za hali hiyo zilianza kujitokeza mapema kabisa pale mwanandugu mmoja alipoenguliwa kwenye kamati hiyo, kwa kile kinachoelezwa, kamati hiyo kufanya jukumu hilo kwa uhuru zaidi.

Apr 12, 2012

Buriani Steven Kanumba: Kifo chako kimenifundisha jambo kubwa mno

Marehemu Steven Kanumba enzi za uhai wake

Steven Kanumba siku alipomtembelea Rais Kikwete
nyumbani kwake mjini Dodoma

WASANII mahiri wa filamu nchini wanazidi kupukutika, wasanii kama Mzee Jongo, Mzee Kipara, Mzee Pwagu, Pwaguzi, Mama Haambiliki na wengine. Lakini msiba wa hivi karibuni uliotokea Jumamosi ya tarehe 7 Aprili umeonekana kuwagusa na kuwashtua wengi sana, wafuatiliaji na wasio wafuatiliaji wa filamu, hasa kutokana na kifo cha ghafla cha kijana ambaye umaarufu wake ulikuwa ukizidi kupanda, na msanii mahiri wa filamu nchini, marehemu Steven Kanumba.

Umati uliojitokeza kuanzia siku kilipotangazwa kifo cha Kanumba hadi mazishi yake ni ushuhuda tosha kwamba tasnia ya filamu ni sekta yenye nguvu kubwa sana na kama ingetumiwa vizuri na serikali ingeweza kuchangia pato kubwa mno.

Apr 11, 2012

Mazishi ya Kanumba yahudhuriwa na maelfu ya watu na kuliza wengi

Steven Kanumba enzi za uhai wake

Elizabeth Michael (Lulu) anayehusishwa na
kifo cha KanumbaPicha zote hapo juu zinaonesha jinsi watu walivyojitokeza
kwa wingi kwenye mazishi ya Msanii wa filamu
Steven Kanumba, kuanzia viwanja vya Leaders hadi
kwenye makaburi ya Kinondoni

Si watu wengi waliotaka kuamini kwamba aliyekuwa mcheza filamu maarufu nchini Tanzania Stephen Kanumba hatunaye tena duniani mpaka pale walipouona mwili wake ukiagwa.

Ilikuwa ni siku ya kipekee, yenye majonzi, simanzi na machozi mengi wakati mamia ya watu wakifurika Jumanne asubuhi kwenye viwanja vya Leaders Club jijini Dar es salaam kuuaga mwili wa aliyekuwa mcheza filamu maarufu nchini Steven Charles Kanumba.

Apr 7, 2012

Mradi wa Swahiliwood


MFDI imejiingiza katika mradi wa kusisimua na wa ubunifu, ikijihusisha katika sekta mahiri ya filamu nchini Tanzania inayokua kwa kuwasaidia watayarishaji wa filamu katika kipengele ambacho kinasimamia masuala ya Elimu kupitia Burudani (Entertainment-Education). 

Mchakato wa uzalishaji filamu utazingatia kujenga uwezo wa watengenezaji filamu wa ndani wa Swahiliwood, na maudhui yao ya kiElimu kupitia Burudani yatawafikia watazamaji mbalimbali kupitia mtandao mkubwa wa usambazaji wa Swahiliwood.

Msanii maarufu wa filamu Steven Kanumba hatunaye tena

Steven Kanumba (1984-2012)

Marehemu Kanumba akipelekwa chumba cha maiti

Elizabeth Michael (Lulu) anayehusishwa na kifo
cha Steven Kanumba

Zifuatazo ni picha za maombolezo:
Wasanii na wapenzi wa filamu wakiwa ndani ya fensi
ya nyumba aliyokuwa akiishi marehemu Kanumba

Wasanii mbalimbali wakiwa na simanzi nyumbani kwa
Steven Kanumba

Mwanamuziki H. Baba akiongea na waandishi wa habari
nyumbani kwa Steven Kanumba

Mohammed Mwikongi (Frank) akiongea kwa uchungu
kuhusu kifo cha Steven Kanumba

Mkurugenzi wa Global Publisher, Eric J. Shigongo
akiwasili nyumbani kwa Steven Kanumba

Mkurugenzi wa Aset, Asha Baraka akieleza masikitiko
yake kuhusiana na kifo cha Steven Kanumba

Ruge Mutahaba naye akielezea masikitiko yake kuhusiana
na kifo cha Steven Kanumba nyumbani kwa marehemu

Msanii maarufu wa filamu  nchini, Steven Kanumba, amefariki dunia ghafla usiku wa kuamkia leo baada ya kudondoka na kujingonga sehemu ya kisogo akiwa nyumbani kwake Vatican, Sinza jijini Dar es Salaam.

Tukio hilo limetokea majira ya saa 7 usiku wa kuamkia leo na taarifa za kudondoka kwa Kanumba zilitolewa na kijana anayeishi naye hapo nyumbani ajulikanaye kwa jina la Seti aliyemwita daktari kujaribu kuokoa maisha yake lakini alipofikishwa hospitali ya Muhimbili tayari alikuwa amekata roho.

Apr 5, 2012

Maadili ya Watanzania katika filamu ni yepi?


SUALA la maadili ya Mtanzania hasa katika filamu limekuwa linazungumzwa sana, na binafsi limekuwa linanitatiza sana kama nilivyokuwa natatizwa na suala la mila na utamaduni wa Watanzania. Kama moja ya makala zangu nimewahi kuuliza maswali haya na sikuweza kupatiwa majibu japo ni kama nilijijibu mwenyewe: Tunaposema utamaduni na mila za Watanzania tunamaanisha nini kwa Tanzania yenye zaidi ya makabila 120 ambayo kila moja lina mila na utamaduni wake? Na huu utamaduni na mila za Watanzania ni upi hasa?


Ndivyo leo ninavyojaribu kuliangalia suala hili la maadili ya Mtanzania kwenye makabila 123 na kujaribu kujiuliza maswali ambayo ninapata majibu nusunusu tu. Niliwahi kumuuliza kiongozi wa Bodi ya Ukaguzi wa Filamu na Michezo ya Kuigiza tulipokutana kuhusu yepi ni maadili ya Watanzania wanayoyaangalia kwenye filamu zetu?