Jun 17, 2012

Tamasha la filamu la wazi kufanyika Tanga Juni 2012


Tamasha kubwa la filamu la wazi linatarajiwa kuanza tarehe 30 mwezi huu, tamasha hilo linajulikana kwa jina la Grand Malt Tanzania Open Film Festival (TOFF) na litafanyika jijini Tanga kwa mara ya nne katika viwanja vya Tangamano, ambapo litadumu kwa muda wa siku saba, na kwa kila siku zitaonyeshwa filamu tatu.

Mkurugenzi wa kampuni ya Sofia Production ya Jijini Dar es Salaam, Mussa Kisoki, amesema kuwa kila kitu kimekamilika kwa ajili ya tamasha hilo ambalo linafanyika kwa mwaka wa nne toka kuasisiwa kwake.

Alisema kuwa tamasha limepokelewa vema kwa Jiji la Tanga na kwa mwaka huu kutakuwa na mambo tofauti sana kwani pamoja na wasanii wa tasnia ya filamu kuwepo katika tamasha hilo lakini pia kuna semina zitaendeshwa kwa siku hizo ambazo ni wasanii na wadau wengi watapata nafasi ya kujifunza kuhusu sheria za hakimiliki na hakishiriki.

Kwa upande wa burudani kutakuwa na vikundi vya ngoma za asili, Tanga Stars na vikundi vingine vya burudani kutoka jiji la Tanga, ambapo siku ya ufunguzi bendi ya taarab ya Tanzania Moto kutoka jijini Dar es Salaam itatumbuiza siku ya ufunguzi wa maonyesho haya ya kihistoria na kipekee.

No comments: