Sep 6, 2011

Marehemu Tabia wa Kidedea afufuliwa

 Marehemu Dalillah Peter Kisinda ‘Tabia’

Pamoja na kutangulia mbele za haki mwanzoni mwa mwaka huu, Watanzania watapata fursa ya kuona vimbwanga vya aliyekuwa mwigizaji mkubwa Bongo, marehemu Dalillah Peter Kisinda ‘Tabia’ katika muvi yake ya mwisho ya Naomi inayokimbiza sokoni.

Kwa mujibu wa mtayarishaji wa filamu hiyo, Hamis Kibari, watakaoitazama muvi hiyo watagundua kwamba Tabia aliyevuma na Kundi la Kidedea alikuwa hazina kubwa ya uigizaji Bongo kwa jinsi alivyomudu vizuri nafasi yake.


“Tabia alifariki dunia wakati tunajipanga kutengeneza ‘part II’ ya filamu hii… Lilikuwa ni pigo kubwa kwetu lakini tumeamua kuwaonesha Watanzania kazi yake ya mwisho kabisa duniani hivyo ni kama ‘amefufuliwa’ upya,” alisema Kibari na kuongeza:

“Mbali na Tabia, Filamu ya Naomi imewashirikisha mastaa wengine kama Bakari Makuka (Beka), Leah Mussa (Shaster) na Suzane Lewis (Natasha).” 


No comments: