Jun 24, 2011

Tamasha la filamu: “Grand Malt Tanzania Open Film Festival” ndani ya Tanga kuanza Juni 27

Mkurugenzi wa Sofia Production, Mussa Kissoky (kulia)
akielezea kwenye ukumbi wa Habari MAELEZO.
Katikati ni Meneja Masoko wa TBL, Fimbo Butallah,
kushoto ni Meneja wa Grand Malt, Consolata Adam

Tamasha kubwa la wazi la filamu nchini Tanzania litakalojulikana kama 'Grand Malt Tanzania Open Film Festival' linatarajiwa kufanyika jijini Tanga kuanzia Juni 27, 2011 ambapo zaidi ya Filamu kumi kali kutoka kwa watayarishaji mahiri wa Tanzania zinatarajiwa kuoneshwa katika tamasha hilo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa kampuni ya
Sofia Production, Mussa Kisoki alisema tamasha hilo litafanyika katika viwanja vya Tangamano, kuanzia Juni 27 na kumalizika Julai 3 mwaka huu.


Alisema tamasha hilo litatoa fursa kwa wadau mbalimbali kukutana na kubadilishana mawazo na kuburudika na vivutio mbalimbali vitakavyosindikiza tamasha hilo. Pamoja na onesho la filamu pia patakuwepo na ngoma za asili na kwamba litapambwa na burudani kutoka kwa wasanii wa muziki wa kizazi kipya na kushuhudiwa na nyota wa filamu mbalimbali.

Lengo la tamasha hilo ni kulikuza na kulitangaza soko la filamu za Kitanzania kwa ajili ya kuongeza ajira kwa vijana waliojiari kupitia filamu hapa nchini

No comments: