Dec 15, 2010

Kikao cha Nane cha Sekta ya Utamaduni kimefanyika Mkoani Mwanza

Jengo la PPF ndani ya ROCK CITY

Prof. Hermans Mwansoko na Gonche Materego
Kikao cha nane cha sekta ya Utamaduni kilifanyika jijini Mwanza hivi karibuni kikiwashirikisha wakurugenzi wa idara, maafisa utamaduni wote nchini na wadau mbalimbali wa utamaduni na kuja na mikakati mbalimbali ya uboreshaji.

Mkurugenzi wa Idara ya Utamaduni, Profesa Hermans Mwansoko alisema kikao hicho kilichobeba kaulimbiu ya Sanaa ni Ajira Tuithamini, kikajikita kwenye uwasilishaji wa mada na machapisho mbalimbali kuhusu sekta ya utamaduni ambapo wajumbe walipata fursa ya kujadili, kuja na changamoto mbalimbali na baadaye kupata majibu na dira ya changamoto hizo.

Sekta ya utamaduni kwa sasa inakua kwa kasi hivyo, nguvu kubwa lazima iwekezwe huko ili kuhakikisha sekta hii inakuwa chanzo kikubwa cha ajira na mapato miongoni mwa Watanzania ikiwa ni pamoja na kulitambulisha taifa katika ngazi mbalimbali za kimataifa.

Mada zilizowasilishwa ni pamoja na; Nafasi ya Sanaa Katika Ajira nchini Tanzania, Ukuaji wa Tasnia ya Filamu, Chachu Katika Kukuza Ajira, Sanaa Endelevu ni Ujasiriamali, Umuhimu wa Mafunzo Katika Ajira ya Sanaa, Mchango wa Utunzaji Kumbukumbu Katika Kukuza Utamaduni wa Mtanzania na ile ya Uzoefu wa Kazi mikoani.

No comments: