Nov 15, 2009

Shirikisho la Filamu Tanzania na Mikakati mipya

Katibu Mkuu, Bishop Hiluka (anayeandika) akijadiliana jambo na Msaidizi wake, 
Simon Mwakifwamba (Jaspa) na mjumbe wa bodi Mike Sangu (aliyesimama) kabla ya mkutano kuanza.

Katika kuonesha kuwa Shirikisho la Watengeneza Filamu Tanzania (TAFF) linajizatiti katika kuhakikisha kuwa fani ya uigizaji wa filamu inasonga mbele, juzi lilifanya mkutano mkubwa na wadau wa filamu katika kuhimiza uanzishwaji wa vyama vya fani husika (kama Chama Cha Waigizaji, Chama Cha waongozaji, Chama Cha Waandishi wa Skripti, n.k).

Hapa ni baadhi ya picha za mkutano huo uliofanyika kwenye ukumbi wa Vijana Social Hall, Kinondoni, tarehe 13/11/2009.

Rais wa Shirikisho Salum Mchoma (Chiki) akihutubia mamia ya wadau waliohudhuria mkutano huo.

Sehemu ya umati wa wadau wakimsikiliza Rais wa Shirikisho (hayupo pichani)

Wadau wakiwa watulivu wakisikiliza kwa makini

Baadhi ya Wasanii wakongwe wakifuatilia kwa makini

Mtunzi wa hadithi mkonge hapa nchini, Mzee Faraji Katalambula pia alikuwepo

Mshereheshaji wa shughuli hiyo, Colleta Rymond akiwa katika pozi

Msanii maaruf wa Bongo Dar es Salaam, Kulwa Kikumba (Dude)

Makamu wa Pili Rais, Jacob Steven (JB) katika pozi akifuatilia kwa makini.

Mdau wa filamu kutoka Zanzibar pia alikuwepo kuwakilisha upande wa pili wa Muungano wa Tanzania. Hapa akijitambulisha kwa wadau.

Mwenyekiti wa Bonanza, Darwesh akiwa makini

Mhamasishaji wa TAFF Joyce Kiria, ambaye pia ni mtangazaji wa kipindi cha Bongo Movie akifuatilia kwa makini.

No comments: