Hans PR

Hans PR

Nov 5, 2009

Ray na Johari wanapogeuka Madaktari!

Zifuatazo ni picha za baadhi ya Wasanii maarufu katika tasnia ya Filamu hapa Tanzania ambazo zimechukuliwa kutoka kwenye filamu moja inayoitwa Pesa (Shekeli) iliyoandaliwa na Kampuni ya Aminaah Entertainment. Sinema hii imekusanya mastaa kibao wa filamu za Kibongo kama vile Ray, Johari, Mainda, Biggie, Sajuki, John Lister, Kaike, na wengineo kibao. Nimebahatika kuiona movie hiyo nilipofika kwenye ofisi za Aminaah lakini nikashangaa kuona kuwa muandaaji kaamua kuihifadhi sinema hiyo stoo tu bila kuiingiza sokoni. Kwa kuwa ni sinema nzuri, nilimuomba aniruhusu japo nichukuwe picha hizi chache ili kuujulisha umma uwepo wa sinema hiyo. Sinema hiyo imepigwa picha na Faraji Rashid na imeongozwa na John Lister.

Ray (Vincent Kigosi) akitoa maelekezo kwa Johari (Blandina Chagula) 
kuhusiana na mgonjwa ambaye hayupo pichani

Johari (Blandina Chagula) akisikiliza mapigo ya moyo ya mgonjwa

Ray akichunguza X-ray hiku Johari akiandaa taarifa

Sajuki (Juma Kilowoko) pia yumo kwenye movie hiyo ya aina yake.

Sajuki akiwa na mgonjwa wake (Faraja) akimuelekeza sehemu 
ya kuketi baada ya kumtoa mimba

Biggie (Lumole Matovolwa) pia yumo kwenye movie hiyo. 
Yeye kacheza kama mmiliki wa hospitali wanayofanya kazi kina Ray

No comments: