Nov 25, 2009

Kuna nini Basata?

Naibu Katibu Mkuu wa TAFF, Simon Mwakifwamba akielezea jambo mbele ya Katibu Mtendaji wa Basata


Leo tarehe 25/Novemba/2009 ni siku ambayo wadau mbalimbali wa filamu, wakiwemo waandaaji, waandishi wa skripti, waigizaji, wapiga picha na wengineo waliamua kuwasindikiza viongozi wao wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) walioongozwa na makatibu Bishop Hiluka na Simon Mwakifwamba kwenda zilipo ofisi za Basata kwa ajili ya kujua hatma ya usajiri wa shirikisho, hii ni baada ya wadau hao kuchoshwa na longolongo za Basata ambazo zimeonekana kuwa na nia ya kuwadhoofisha.
 

Kilio cha wadau hawa siku zote kimekuwa ni kuungana pamoja na kufanya kazi kwa mshikamano ili kuboresha kazi za filamu za Kitanzania, lakini kumekuwepo na watu wachache wanaoonekana kuwa hawautaki umoja huu na wako tayari kuudhoofisha kwa nguvu zote. Hapa chini ni baadhi ya picha za wadau hao waliofika Basata kujua hatma yao, ambapo Katibu Mtendaji wa Basata ameahidi kulishughulikia suala hilo.

Katibu mtendaji wa Basata, Ghonche Materego akielezea jambo huku wadau wakimsikiliza kwa makini

Baadhi ya viongozi wa shirikisho na wafanyakazi wa Basata wakimsikiliza Katibu Mtendaji wa Basata

Wanahabari nao hawakubaki nyuma katika kuhakikisha wanapata habari anazozihitaji. Walikuwepo wanahabari kutoka Star TV na Channel 5.


Baadhi ya wadau wakiwa nje ya jengo la Basata wakisubiri kujua hatma ya shirikisho lao linalopingwa na Basata, wakati huo kulikuwa na kikao cha viongozi wa shirikisho na Basata ndani.


Hapa wadau wakisubiriana ili kuingia ndani ya majengo ya Basata kwa pamoja huku wakipanga mikakati kabla ya kuingia Basata


Baada ya kikao na Katibu Mtendaji wa Basata, wadau wanaonekana wakisubiri kwa hamu kusikia kutoka kwa viongozi wao. Mtu mfupi anayeonekana ni msanii maarufu wa kundi la Kaole, Mlopelo


Wadau wakijadiliana nje ya jengo la Basata baada ya kikao na Katibu Mtendaji wa Basata. Hapa nyuso za wadau hawa zikionesha matumaini makubwa.

No comments: