Nov 15, 2009

Kumekucha Bonanza la Wadau wa Filamu viwanja vya Leaders Club

Bonanza la Wadau wa Filamu hapa Tanzania linalofanyika kila jumamosi kwenye viwanja vya Leaders Club, Kinondoni linazidi kunoga. Hapa ni baadhi ya picha za matukio mbalimbali zilizochukuliwa Jumamosi ya tarehe 14/11/09.

Msanii Maarufu wa Kaole, Mlopelo akijimwaga kusakata dansi na mwanadada.


Baadhi ya umati uliofurika kupata burudani

Mwenyekiti wa Bonanza, Darwesh akiwa na baadhi ya wakongwe wa burudani akiwemo Mzee Makassy (aliyeshika gazeti)

Yvonne Cheryl (Monalisa) katika pozi na Ndumbwagwe Misayo (Thea)

Msanii maaruf Haji Adam akionesha namna ya kusakata mayenu

Jacob Steven (JB) pia hakuwa nyuma kusakata mayenu

Kulwa Kikumba (Dude) pia alijitosa uwanjani

Chiki Mchoma alidhihirisha kuwa anaweza pia kuimba

Hapa ni baadhi ya mabinti waliojitosa kushindana katika shindano la kumtafuta mkali wa kucheza

Jacquiline Wolper na Kelvina wakidhihirisha kuwa wanaweza

No comments: