May 24, 2012

Soko huria na filamu za Bongo


Men's Day Out

Aching Heart

Glamour

Uchumi wa soko huria Bongo karibuni umechangia kukua kwa sinema  za Kiswahili. Ukipita mitaani Bongo unakutana na filamu kila kona. Si kama miaka ileeee… tukililia sinema hatuzioni… Imekuwa kama mchezo  bila refa, mkutano bila mwenyekiti, darasa bila mwalimu, nyumba bila mzazi…

Wafanyabiashara wanaahidi milioni kumi hadi ishirini kwa sinema; watoaji wanalipua; waigizaji hawalipwi vizuri; utengenezaji sinema unafanywa haraka haraka.  Sinema zinatolewa ndani ya mwezi mmoja. Haraka haraka…

Wasanii wanaigiza bila mazoezi, baadhi ya watengenezaji wanakula  ngono na wasichana wazuri wazuri, sinema zinazotolewa eti zinalinganishwa na za Wanaijeria.  Tangu lini  sinema za Wanaijeria zikawa kipimo cha filamu zetu?

Pia Watanzania hatupendi au hatununui sinema zinazotolewa na Wabongo wenzetu. Kisa? Hazituvutii. Moja ya sababu ni kwamba zinatengenezwa vibaya kwa kulipuliwa.  Sinema ikitengenezwa vizuri tuinunue, tuifurahie, tuitolee maoni na kuitangaza. Hiyo ndiyo njia kuu itakayotufanya tuendelee kama wenzetu, tunaowaona Miungu kutuzidi.

Tukumbushane kwamba sinema ni sanaa inayochukua muda. Huwezi kufanya sinema kwa mwezi mmoja...

No comments: