Feb 17, 2011

Wahujumu wa kazi za Wasanii waanikwa mkoani Pwani

 Kazi feki za sanaa zikiwa tayari kwa kuuzwa

Kazi feki zikitayarishwa kuchomwa huko China

Kundi la watu ambao wamekuwa wakihujumu kazi za wasanii mbalimbali nchini limebainika mkoani Pwani. Uchunguzi uliofanywa kwa muda mrefu katika magulio kadhaa ya mkoa wa Pwani umebaini kuwapo kwa kundi kubwa la wafanyabiashara wanaouza kazi za Wasanii mbalimbali zilizodurufiwa (duplicated) kwa bei ya chini na kusababisha wasanii kutofaidika na kazi zao.

Uchunguzi huo wa muda mrefu katika wilaya za Bagamoyo, Kisarawe, Rufiji na Mkuranga umebaini kuwapo kwa wauzaji hao wa kazi za wasanii ambao wamekuwa wakidurufu na kuziuza kazi hizo kwa bei ya chini ya shilingi 1000.

Miongoni mwa kazi ambazo zimekuwa zinaongoza kwa kuuzwa kwa wingi katika magulio hayo ni kazi za muziki wa injili za Rose Mhando na video za filamu za wasanii ambazo nyingi zimechezwa na wasanii nguli; Vincent Kigosi "Ray", Steven Kanumba na Blandina Chagula "Johari".

Source: Mtanzania

No comments: