Feb 17, 2011

Shirikisho la Filamu Tanzania laitaka serikali kuwekeza kwenye filamu



Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) limeitaka serikali kuwekeza katika kazi za sanaa ya muziki na filamu ili kukuza pato la taifa. Hayo yalisemwa na Rais wa sirikisho hilo, Simon Mwakifwamba, katika uzinduzi rasmi wa shirikisho hilo ulioambatana na Tamasha la Filamu za Kitanzania “The Mwalimu Nyerere Film Festival” lililoanza Februari 14 katika viwanja vya Leadres Club vilivyopo Kinondoni, jijini Dar es Salaam.

Tunaiomba serikali iliangalie hili, kwani sekta ya sanaa ina mapato makubwa sana ambayo yanaweza kuiendesha nchi iwapo serikali italizingatia hili. Si hivyo tu bali itaweza kutukomboa wasanii kwa namna moja ama nyingine kutokana na wizi ambao umeeenea hivi sasa,” alisema.

Alisema kuwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) inapaswa kuzingatia na kuhakikisha mapato yatokanayo na sanaa ya muziki na filamu yanapatikana, kuliko kuwaachia wachache ambao wananeemeka kwa kuwafaya wasanii kurudi nyuma huku serikali ikikosa mapato.

Alisema kwa sasa shirikisho hilo lipo katika wakati mgumu na kuiomba serikali iwasaidie hasa kwa vile wanategemea kufanya tamasha kubwa la filamu baadaye Septemba mwaka huu.

Source: Mwananchi

No comments: