Feb 21, 2011

ARTERIAL Network: Mtandao wa wasanii uliozinduliwa Tanzania

 Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo wa Zanzibar, 
Abdillah Jihadi aliyekuwa mgeni rasmi siku ya uzindua 
wa Mtandao wa ARTERIAL Tanzania. Wengine ni 
Mwenyekiti mpya wa Mtandao huo nchini, Laurian Kipeja (kati) 
na kushoto ni mwakilishi wa Mtandao huo kwa Afrika, 
Telesphore Mbabizo.

Picha ya pamoja na Mgeni Rasmi.
Baadhi ya wajumbe waliohudhuria mkutano wa uzinduzi wa Mtandao wa ARTERIAL Tanzania

Mtandao wa wasanii Barani Afrika unaojulikana kwa jina la ARTERIAL Network, umezindua tawi lake nchini Tanzania na tayari umepata viongozi watakauongoza kwa kipindi cha miaka mwili. Uzinduzi wa mtandao huo ulifanywa na Waziri wa Habari, Utamaduni na Utalii wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) Mh. Abdillahi Jihadi, katika hoteli ya Zanzibar Grand Palace.

Mmoja wa viongozi waliochaguliwa kuuongoza mtandao huo kwa kipindi cha miaka miwili ni Katibu Mkuu wa Chama cha Waandishi wa Habri za Sanaa na Utamaduni Tanzania (CAJA), Hassan Bumbuli, aliyechaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa mtandao huo, huku aliyekuwa mratibu wa kamati ya muda ya mtandao huo Tanzania, Laurian Kipeja akichaguliwa kuwa Mwenyekiti.

Wengine ni Ali Bakari aliyechaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti, na wajumbe watano wanaowakilisha sekta mbalimbali za sanaa ikiwemo muziki, sanaa za maonesho, sanaa za ufundi, filamu na sekta ya habari.

Wajumbe waliochaguliwa na nafasi zao kwenye mabano ni pamoja na Sauda Simba Kilumanga (Muziki), Godfrey Lebejo Mngereza (sanaa za maonesho), Sabrina Othman (filamu), sharifa Juma (Sanaa za Ufundi) na Sofia Ngalapi (Habari).

No comments: