Feb 8, 2011

Steps na Pilipili Entertainment kwenda kimataifa

 Nembo ya filamu ya nchi za Caribbean

Nembo ya Tamasha la Filamu Zanzibar

Poster ya filamu ya Deception

Kampuni ya usambazaji wa filamu ya Steps Entertainment na ile ya utengenezaji filamu ya Pilipili Entertainment ziko mbioni kupata soko la kimataifa kutokana na filamu zao kunadiwa katika tamasha la kimataifa la Fair International Film Festival sambamba na Iran Film Market. Taarifa za kampuni hizi zimetolewa na Meneja wa Zanzibar International Film Festival (ZIFF), Daniel Nyalusi, kuwa Iran watatumia filamu za kampuni hizo kupata soko la kimataifa.

Kwa mujibu wa Ziff, wanajaribu kupata wasambazaji, wazaalishaji na wawekezaji wa filamu duniani, ambao wangependa kununua, kusambaza, kutengeneza au kufanya kazi ya pamoja na kiwanda cha filamu hapa nchini.

No comments: