Feb 1, 2011

Wasanii Tanzania wanatakiwa kujifunza Kiingereza

Christina Innocent "Mama Bishanga" (kushoto), 
na mwanae Hendrick Nambira "Kenny" (kulia), 
akizungumza na Waandishi wa Habari ambao 
hawapo kwenye picha, kwenye ukumbi wa 
Habari MAELEZO


 Wasanii maaruf wa sinema Tanzania, 
Vincent Kigosi (Ray) na Steven Kanumba

Emmanuel Myamba, mmoja wa waigizaji wa filamu nchini wanaoijua vizuri lugha ya Kiingereza

Wasanii wa sanaa za maonesho na filamu nchini wametakiwa kuongeza bidii kujifunza lugha ya Kiingereza ili waweze kupanua wigo wa soko la kazi zao kimataifa. Mwito huo ulitolewa jijini Dar es Salaam siku ya Jumatatu na msanii maaruf wa maigizo nchini, Christina Innocent maaruf kwa jina la Mama Bishanga, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hali ya sanaa hapa nchini.

Mama Bishanga ambaye kwa sasa anasomea shahada ya shughuli za kijamii nchini Marekani, alisema kuwa kazi za sanaa za Tanzania hazionekani katika nchi za nje hususan Marekani ikilinganishwa na kazi za nchi nyingine kutokana na tatizo la lugha.

Kazi za wasanii wa nchi zote duniani zinatumika sana nchinini Marekani, watu wananunua lakini nimefanya utafiti nimeona kazi za hapa kwetu nazo zipo kule lakini hazina soko,” alisema.

Kwa hali wasanii hawana budi kukubali kuingia darasani kujifunza lugha ya Kiingereza, bila kupoteza nafasi ya lugha ya Kiswahili katika sanaa.

1 comment:

Anonymous said...

Habari Mkubwa? Sanaa ni njia moja wapo ya mawasiliano kwa njia yoyote, sanaa hiyo ndiyo inayofanya wasanii kwa kutumia lugha yoyote, kama kiingereza ni sehemu ya kufanya kazi nzuri watu mashuhuri, kama James Cameroon kubuni lugha na kutumia ktk filamu yake ya Avatar kama kiingereza ni muhimu kulikuwa na sababu gani ya kutumia lugha ya kubuni? Nakumbuka nilipokuwa nchini Sweden Niligundua kuwa Watanzania wamekuwa watumwa kwa kuamini wakijua Kiingereza ndiyo kila kitu, lakini ni utumwa kwani unapotua Sweden Kiingereza hakina maana na ndiyo maana wao wamefanikiwa kwa sababu ya kutumia lugha yao wanayoijua kuliko kukariri kugha za kigeni. Angali upya njia mbadala ktk kubororesha filamu na si Lugha.