Oct 25, 2009

Umewahi kusikia juu ya KITI CHEUPE?

Florian L. Mtaremwa (Ray) akiwa kwenye ofisini zake katika studio ya RAV ProductionOfisi hiyo ipo eneo la Malapa, Ilala.

Florian Lawrence Mtaremwa (maarufu kama Ray wa Splendid), Mkurugenzi na mmiliki wa kampuni ya RAV Production ameamua kuja kivingine katika sanaa ya filamu ya Bongo baada ya kutunga na kuandaa sinema ya kusisimua inayoitwa 'White Chair' au Kiti Cheupe kwa Kiswahili. Sinema hiyo ni ya aina yake katika nchi hii ambayo unaweza kuifananisha na sinema kali za Hollywood kama vile Anaconda na nyingine za kusisimua ambazo zitakufanya usikae vizuri kwenye kiti chako pindi uziangaliapo.


Kwa mujibu wa maelezo ya mtunzi huyo ni kwamba; kisa au hadithi ya sinema ya Kiti Cheupe ni kuhusiana na kosa kubwa sana lililofanywa na mmoja wa wakazi wa eneo fulani lililopelekea wakazi wote wa eneo hilo kupata adhabu kali kutoka kwa Kiti Cheupe...

Hapa chini ni baadhi ya picha zinazowaonesha wakazi wakipata adhabu kutoka kwa Kiti Cheupe...
 
Unaweza kuwasiliana na mtayarishaji mwenye picha iliyo juu:
Florian Lawrence Mtaremwa
Hotline: +255 713 619971

No comments: