Jun 12, 2015

Sir Christopher Lee, nyota wa filamu ya Dracula afariki

Moja ya scene alizocheza hayati Christopher Lee
Sir Christopher Lee
Mwigizaji wa siku nyingi na nyota wa filamu zilizopendwa na wengi, Sir Christopher Lee, amefariki akiwa na umri wa miaka 93. Msanii huyo ambaye jina lake kamili ni Christopher Frank Caradini Lee alizaliwa mnamo mwaka 1922, alikuwa mwigizaji wa filamu na mchekeshaji mzaliwa wa Uingereza aliyejenga jina lake kwa kuigiza katika filamu ya Dracula na Frankenstein katika filamu ya kutisha aligiza katika zaidi ya filamu 250.

Alijulikana sana kwa kuigiza kama Scaramanga katika filamu ya James Bond na Evil Wizard Suriman katika filamu ya Lord of the Rings. Msanii huyo pia ameigiza katika filamu za The Wicker Man na Stars wars. Imeripotiwa kuwa mwigizaji huyo alifariki siku ya Jumapili katika hospitali ya Chelsea Westminster mjini London baada ya kulazwa akiugua ugonjwa wa tatizo la mapafu na moyo.


No comments: