Jun 5, 2015

Hiroshi Koizumi, mwigizaji wa filamu za Godzilla afariki dunia akisumbuliwa na homa ya mapafu

Hiroshi Koizumi, enzi za uhai wake
Moja ya sinema za Godzilla
Hiroshi Koizumi, msanii wa Japan ambaye aliigiza katika filamu nyingi za Godzilla amefariki akiwa na umri wa miaka 88. Kulingana na ripoti, alifariki mjini Tokyo tarehe 31 Mei 2015, kutokana na homa ya mapafu (Pneumonia) katika hospitali ya Tokyo.

Koizumi aliigiza kama Godzilla katika filamu ya ‘Godzilla Raids Again’ ikiwa ni filamu ya kwanza ya Godzilla. Baadaye aliigiza katika filamu kadhaa za kutisha ikiwemo ‘Mothra’, ‘Godzilla vs The Thing’ na ‘Ghindorah and the Three headed Monster’.


Hiroshi Koizumi alizaliwa tarehe 12 Agosti 1926, alikuwa muigizaji wa Japani, na sinema alizowahi kucheza ni pamoja na:
- Godzilla Raids Again (1955) – Shoichi Tsukioka
- Song for a Bride (1958)
- Mothra (1961) – Dr. Shinichi Chujo
- 47 Samurai (1962)
- Matango (1963)
- Atragon (1963)
- Mothra vs. Godzilla (1964) – Professor Miura
- Dogara, the Space Monster (1964) – Kirino
- Ghidorah, the Three-Headed Monster (1964) – Professor Miura
- Ultra Q (1966; TV series)
- Godzilla: Tokyo S.O.S. (2003) – Dr. Shinichi Chujo


No comments: