Jun 17, 2015

Sekta ya Filamu duniani inahodhiwa na Wayahudi

Mtengeneza filamu wa Hollywood, Steven Spielberg
KATIKA zama zetu hizi, sinema ni chombo muhimu sana kinachotumiwa kueneza utambulisho, utamaduni na fikra. Mfano maalumu wa uwekezaji mkubwa katika sekta ya sinema duniani ni uwekezaji wa Wamarekani na Waisrael (Wayahudi) katika sekta ya filamu. Wakati wengine wamelala, Wayahudi walifahamu mapema sana taathira ya sekta ya sinema na umuhimu wake katika propaganda na ili kuidhibiti sekta hii walitumia uwezo wao wote.

Katika miaka ya karibuni Serikali ya Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran wameonekana kuanza kuzinduka katika usingizi na kuanza kujipenyeza kwenye sekta ya filamu duniani ili kueneza utambulisho na tamaduni za Kiislamu dhidi ya tamaduni za Kimagharibi, lakini bado wana kazi ngumu sana kufuta alama zilizoachwa na sinema za Hollywood, chini ya udhibiti wa Israel na Marekani.

Picha ya tukio la Holocaust (mauaji ya kimbari ya Wayahudi
wakati wa utawala wa Nazi wa Hitler)
Iran kwa miaka ya karibuni imegundua kuwa sekta ya sinema si njia nzuri tu kwa kueneza utamaduni na utambulisho, bali pia ni njia nzuri zaidi ya kueneza fikra zao (propaganda) dhidi ya fikra wanazodhani si sahihi. Wizara ya Utamaduni na Mwongozo wa Kiislamu, Shirika la Utangazaji la Iran (IRIB) na wasanii wa nchi hiyo wameamua kuwekeza zaidi katika medani ya sinema. Yote hii ni kujaribu kuzijibu Israel na Marekani.

Mwanzoni mwa kudhihiri sekta ya filamu duniani, Wayahudi walitoa misaada mikubwa ya kifedha (kwa kusaidiwa na Marekani) kwa sekta hiyo muhimu kwa lengo la kutekeleza malengo yao. Kwa hivyo baada ya muda walinunua mashirika mashuhuri ya kutengeneza filamu duniani na hasa Marekani ili kuweza kudhibiti na kuhodhi utengenezaji filamu hasa katika nchi za Magharibi.

Ni kwa sababu hii ndiyo hivi sasa aghalabu ya mashirika ya kutengeneza filamu Marekani yanamilikiwa na Wayahudi. Kwa msingi huo mbali na kupata faida kubwa itokanayo na uuzaji filamu, Wayahudi wanatumia filamu kama sehemu ya kueneza fikra zao duniani.

Kwa mfano ushawishi wao katika Hollywood ni mkubwa kiasi kwamba tukio kama la Holocaust (mauaji ya kimbali ambapo Waisrael milioni sita waliuawa na utawala wa Nazi wa Adolf Hitler) sasa limebadilika na kuwa nadharia inayokubalika Hollywood na kila mtengeneza filamu ambaye anafanyia kazi nadharia hiyo anapata uungaji mkono mkubwa wa kifedha kutoka kwao. Uungaji mkono huu huanza tokea wakati wa utengenezaji filamu hadi inapopigiwa debe katika vyombo vya habari ili kuoneshwa katika kumbi za sinema kote duniani (box office).

Mfumo unaotumika kusambaza filamu katika sekta za filamu zilizoendelea, kama Marekani na nchi zingine tajiri huanzia kwenye ‘box office’. Huu ni mfumo maalum ambapo watu hununua tiketi kwa ajili ya kuona sinema ndani ya kumbi za sinema, na baadaye sinema hizo hutolewa kwenye video, kurushwa kwenye vituo vya televisheni za kulipia, kisha katika televisheni za umma, na hatimaye kutolewa kama bidhaa rasmi (DVD) kwa matumizi ya nyumbani. Hapa Tanzania hatuna mfumo huu.

Hata katika medani za mashindano katika tuzo na matamasha ya filamu duniani, kama Oscar nk, Wayahudi huhakikisha kuwa filamu wazitakazo ndizo zinazopata zawadi bora zaidi.

Neal Gabler, mwandishi Myahudi katika kitabu cha ‘An Empire of Their Own: How the Jews Invented Hollywood’ (Ufalme Wao Binafasi: Namna Wayahudi Walivyobuni Hollywood) ameashiria kuwa kuna studio kadhaa kubwa za kutengeneza filamu Hollywood zinazomilikiwa na Wayahudi. Kati ya studio au mashirika hayo ni pamoja na Colombia, Metro Golden-Mayer, Warner Brothers, Paramount, Universal na Fox.

Norman F. Cantor mhadhiri wa Chuo Kikuu cha New York katika utafiti alioufanya mwaka 1994 aliashiria nukta hii kuwa, utengenezaji na usambazaji filamu Hollywood katika miaka 50 ya awali ulikuwa chini ya udhibiti wa Wayahudi wahamiaji na hivi sasa pia sehemu kubwa ya sekta ya burudani Marekani (kwa maana ya sekta za sinema na muziki) inahodhiwa na utawala wa Wayahudi.

Ushawishi huu hasa unajumuisha pia kuwaunga mkono wacheza filamu wenye asili ya Kiyahudi kiasi kwamba leo huko Hollywood kuna idadi kubwa ya wacheza filamu na watengeneza filamu Wayahudi ambao wanaunga mkono utawala wa Israel. Kwa hivyo mbali na kuwa utawala wa Israel unawaunga mkono wasanii hao, vilevile wasanii hao binafsi wanalazimika kueneza na kutangaza fikra za Israel.

Watengeneza filamu waungaji mkono Utawala wa Israel ni pamoja na Erich von Stroheim, Fritz Lang, Roman Polanski, Steven Spielberg na Samuel Goldwyn. Watengeneza filamu hawa ambao baadhi wameshafariki si tu kuwa ni waungaji mkono Israel bali pia athari zao zilikuwa na lengo la kutangaza fikra (propaganda) za Kiyahudi.

Je, ni kitu gani kilichozingatiwa katika filamu hizi na ni maudhui yepi yaliyopewa umuhimu katika filamu zinazounga mkono utawala wa Israel?

Steven Spielberg, mtengeneza filamu Mmarekani aliingiza tukio la Holocaust katika filamu yake ya mwaka 1993 iliyopewa jina la ‘Schneider’s List’ (kwa Kiswahili unaweza kuita Orodha ya Schneider). Kwa miaka mingi kupitia taasisi ya Kiisrael ya SHOA, Spielberg alifanya bidii kukusanya hadithi zinazohusiana na tukio la Holocaust. Aidha alishirikiana na taasisi nyingi za kielimu kuhusiana na suala hili.

Karen Polak mkurugenzi wa moja kati ya taasisi alizoshirikiana nazo Spielberg anasema lengo la filamu kama ‘Schindler’s List’ ni kutoa mafunzo kwa ajili ya kuhakikisha kuwa vizazi vijavyo vina maelezo kamili kuhusu kadhia ya Holocaust.

Kwa mujibu wa nyaraka za kihistoria sambama na kubuniwa utawala wa Israel mwaka 1948 uzingatiwaji sekta ya sinema na Wayahudi pia ulianza kwa mpangilio maalumu. Kwa miaka mingi Wayahudi wamekuwa wakijipenyeza nyuma ya pazia katika nafasi muhimu za uongozi Hollywod ili waweze kudhibiti mkondo wa utengenezaji filamu duniani.

Pamoja na hayo hawakuwa wanajihusisha moja kwa moja katika masuala ya sinema kimataifa. Lakini kutoka mwaka 2000 hadi sasa, filamu ambazo hutengenezwa katika ardhi ya Israel na maeneo ya Palestina yanayokaliwa kwa mabavu zimekuwa zikishirikishwa katika matamasha ya kimataifa. Kwa hivyo Wayahudi sasa wanajitokeza waziwazi katika sekta ya filamu duniani.

Kufanyika kwa ‘Matamasha ya Filamu za Israel’ katika miji ya Los Angeles, Miami na New York ni mfano wa kujitokeza wazi kuwa Wayahudi wameingia rasmi katika sekta ya filamu. Matamasha haya hufanyika kwa ushirikiano wa Utawala wa Israel na Marekani ambapo filamu zilizotengenezwa Israel huoneshwa.

Jambo ambalo limebainika ni kuwa harakati hizi haziishii tu katika kueneza fikra za Israel. Mwaka 1993, utawala wa Israel ulianzisha New Foundation for Cinema and Television (Taasisi ya Mpya ya Israel ya Sinema na Televisheni). Kupitia taasisi hii, Israel inakusudia kueneza ushawishi wake katika soko la sinema duniani. Taasisi hii yenye bajeti kubwa ya kifedha inajitahidi sana kuwavutia watengeneza filamu Waarabu.


Wataalamu 40 wa sinema Palestina akiwemo Aliya Suleiman, Rashid Masharawi na Hany Abu-Assad walitoa taarifa na kukosoa vikali mchezo huu wa kipropaganda wa Israel. Pamoja na kuwepo malalamiko hayo Wayahudi wanaendelea kuwekeza katika taasisi hiyo ili kueneza sera zao duniani.

No comments: