Nov 19, 2010

Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) latoa lawama kwa waandishi wa habari

 Mzee Omari Mayanga akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani)

Bango la Jukwaa la sanaa

Gonche Materego, Katibu Mtendaji wa Basata akifafanua kwenye Jukwaa la Sanaa

Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limewaangushia lawama waandishi wa habari nchini kuwa wamekuwa wakisusia vikao vya Jukwaa la Sanaa vinavyofanyika kila Jumatatu katika ukumbi wa Baraza. Lawama hizo zimetolewa na mwakilishi wa baraza hilo, Mzee Omari Mayanga alipokuwa akiliwakilisha baraza hilo wakati viongozi wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) walipokuwa wakielezea mikakati yao kwa waandishi wa habari kuhusiana na tamasha la filamu la Mwalimu Nyerere.

 Sehemu y umati wa wadau siku ya Jukwaa la Sanaa

Mzee Mayanga aliyasema hayo alipopata nafasi ya kuongea na kusisitiza kuwa wakati Jukwaa hilo linaanzishwa waandishi wengi sana walikuwa wakihudhuria lakini kadri siku zilivyokuwa zikienda idadi yao ilianza kupungua taratibu. Mzee Mayanga aliwaomba waandishi kuhudhuria kwani hapo ndiyo mahali pekee wanapoweza kupata habari mbalimbali za sanaa ili waweze kuihabarisha jamii.

1 comment:

Anonymous said...

Inawezekana nyinyi hamtoi mshiko, waandishi wanapenda sehemu zenye mshiko.