Nov 10, 2010

Filamu za Kibongo zinavyoibwa nje ya nchi

Moja ya filamu za Kitanzania, Black Sunday

Filamu ya One by One iliyotengenezwa na Mahsen Awadh, "Cheni" 

Kwa inasikitisha sana kuona wasanii na watengeneza filamu wa Kitanzania wanavyohangaika kujitengenezea sinema kwa pesa za kubangaiza au pengine za mkopo wakitegemea kuuza na kupata faida itakayowawezesha kupiga hatua kimaisha lakini inatokea kwamba watuwengine wanawaibia. Tena inauma sana endapo mtu huyo anayeiba ni tajiri mkubwa.

Kuna mtandao mmoja ambao wasomaji wanapaswa kuufahamu ambao umekuwa ukitumiwa na watu walio nje ya nchi hasa nchi za ng'ambo ku-download filamu za Kitanzania na kuziangalia bila hata kuwalipa wenye kazi hizo. BOFYA HAPA kuuona mtandao huo unaoonesha sinema za Tanzania na Afrika Mashariki bila hata kuwalipa wenye kazi hizo. 

Niliwahi kumuuliza muigizaji maarufu, Steven Kanumba kama alikuwa na taarifa yoyote kuhusu mtandao huo na kama alikuwa analipwa chochote baada ya kazi zake kuoneshwa kwenye mtandao huo, kwanza alishtuka sana kusikia habari hizo na kuniomba nimpatie anwani ya mtandao huo ili aone kabla hajanijibu. 

No comments: