Nov 23, 2010

Serikali imeombwa kuinua vipaji

Lisa Jensen

Serikali kupitia baraza lake la sanaa (Basata) imetakiwa kuinua vipaji vya wasanii nchini kwa kuweka wawakilishi kwenye ofisi zake za kibalozi zilizoko nje. Ushauri huo ulitolewa na msanii na mwanaharakati wa sanaa, Lisa Jensen, katika mkutano unaowakutanisha wadau mbalimbali wa sanaa kila Jumatatu, safari hii walikuwa wakijadili kuhusu fursa za wasanii.

Lisa Jensen ambaye aliwahi kuwa mrembo wa Kanda ya Ziwa na mrembo namba tatu wa Tanzania alieleza kuwa tatizo linalokwamisha taaluma hiyo ni kukosa msukumo wa serikali kwani imebainika kuwa wasanii wa Tanzania wanapokuwa nje ya nchi wanakosa maslahi mengi kutokana na uwakilishi mbovu kutoka balozi zilizoko nje.

Aidha wasanii wametakiwa kuungana pamoja ili kuikuza tasnia hiyo ya ubunifu ili kutoa nguvu kwa wadau wote wa sekta hiyo na kuiomba serikali kuipa kipaumbele.

1 comment:

Anonymous said...

I see, nimefurahishwa zaidi na hiyo picha ya mrembo. Mmh, sina cha kuongeza