Jan 5, 2011

Watanzania nunueni filamu halisi

Prof. Martin Mhando akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani)

Sharo Milionea, moja ya kazi za Tanzania

MKURUGENZI wa Tamasha la Filamu la Nchi za Jahazi la Zanzibar (Zanzibar International Film Festival), Prof. Martin Mhando, amewataka Watanzania kujitokeza na kununua kazi halisi ili kukuza soko na uchumi wa nchi. Prof. Mhando alitoa wito huo alipozungumza na waandishi wa habari ndani ya ukumbi wa Ngome Kongwe mjini Zanzibar.

Alisema kuwa tayari wasanii wa Tanzania wameweza kupiga hatua katika kutoa filamu mbalimbali, ambazo nyingi kati ya hizo zina mafundisho.

Mbali na hilo, pia alishahuri Tanzania kuundwe Kamisheni ya Filamu, ambayo itasaidia kuiletea nchi matunda mazuri, huku bodi ya filamu iliyoundwa ikiendelea kusimamia ushauri na kamati mbalimbali za maadili.

Alisema, ukinunua nakala halisi unaongeza kipato cha serikali na hata kwa wasanii na wananchi kwa ujumla

No comments: