Jan 25, 2011

Wasanii wapewa elimu ya sanaa, wahamasishwa kupima UKIMWI

Mkurugenzi Mtendaji wa Parapanda Theatre Lab Trust, 
Mgunga Mwa Mnyenyelwa akiongea kwenye Jukwaa la Sanaa

Baadhi ya washiriki wa Jukwaa la Sanaa

WASANII mbalimbali wakiwemo wacheza filamu, wachoraji, wanamuziki na  wachongaji vinyango na sanamu, Jumatatu wiki hii kwenye Jukwaa la Sanaa wamepata elimu ya sanaa ya maonesho  na kuhamasishwa kupima afya zao na jinsi ya kuepuka kukumbwa na ugonjwa wa ukimwi.

Akizungumza kwenye Jukwaa la Sanaa linalofanyika kila Jumatatu katika ukumbi wa Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), Mkurugenzi Mtendaji wa Parapanda Theatre Lab Trust, Mgunga Mwa Mnyenyelwa, amewataka wasanii wote kuwa na dira katika kazi zao kabla ya kutoa kazi, akawataka wafanye utafiti ili kujua kile wanachokifanya kama kitanufaisha taifa.


Aidha aliendelea kusema kuwa kikundi hicho kina malengo ya kuwasaidia wasanii wa Bongo Fleva ili waweze kuimba nyimbo zao zikiwa na mguso wenye asili ya Kiafrika kwa lengo la kuzitofautisha na za nchi nyingine.

Naye, mshauri kutoka shirika la AMREF, Bahati Mwitula, aliwapa somo wasanii hao na kuwahamasisha kupima afya zao ambapo alisema kuwa shirika hilo limeamua kuwafuata watu pale walipo na siyo mpaka watu wawafuate wao.

No comments: