Jan 24, 2012

Swahiliwood - Part 1 - An Introduction
Ilikuwa ni  Jumanne ya tarehe 22 Novemba hadi Jumamosi tarehe 26 Novemba, warsha ya siku tano ambayo ni ya kwanza katika mkakati maalum uliowekwa na taasisi ya Media for Development International – Tanzania (MFDI-Tanzania), kuhakikisha kuwa tasnia ya filamu nchini “Swahiliwood” kama ambavyo wanapenda ijulikane, inafikia kile ambacho tasnia zingine duniani zimeweza.


Washiriki 25 walihudhuria warsha hiyo, wakiwemo watayarishaji wa filamu maarufu na waandishi maarufu wa script. Mimi nilikuwa mmoja wao. Washiriki wengine maarufu waliohudhuria ni pamoja na Jacob Steven (JB), Mahsen Awadhi (Cheni), Suzanne Lewis (Natasha), George Tyson, Hamisi Kibari, John Lister, Ali Yakuti (ambaye hakumaliza mafunzo), Ali Mbwana (Bashiri Mpemba), Chrissant Mhengga na wengineo.Semina hii ilikuwa ya ushindani kwa washiriki kabla ya uteuzi wa pande mbili kwa ajili ya mfululizo wa warsha za uandishi wa script. Tayari wamechagua watu sita ambao wamekidhi viwango na matarajio yao, nitayaleta majina yao baadaye, lakini mimi ni mmoja wa hao walioshinda mtihani huu wa kwanza.


Lengo kuu lilikuwa: 
1. Kutoaa habari za kina juu ya Mradi maalum wa Swahiliwood, na malengo ya mradi huo.
2. Kutoa mafunzo ya jinsi ya kuandika kwa kina kuhusu Mawasiliano na Mabadiliko ya Tabia (Behavior-Change Communication). 
3. Kuwapa ufahamu washiriki wa malengo ya mawasiliano ya Mradi wa Swahiliwood.

1 comment:

Magembe R. Malima said...

Tuinategemea mafunzo haya yatachangia kuboresha filamu zetu ambazo zimekuwa zikilalamikiwa kwa kuwa na miongozo hafifu.