Jan 11, 2012

Mzee Kipara hatunaye tena...

Mzee Said Fundi enzi za uhai wake

Picha hii inamuonesha alipokuwa anaumwa


Mzee Said Fundi, aliyekuwa maarufu kama Mzee Kipara, msanii ambaye amedumu katika sanaa kwa miaka mingi sana amefariki dunia asubuhi saa mbili leo Jumatano tarehe 11 Januari, 2012. Mwanaharakati na mwanamuziki wa siku nyingi, John Kitime, anasema alimfahamu Mzee Kipara kwanza akiwa mwigizaji katika magazeti ya picha yaliyokuwa yakiitwa FILM TANZANIA, baadaye walikutana 'live' akiwa TT katika treni ya reli ya kati.Mzee Kipara pia alikuwa maarufu sana na sauti yake nzito ya kibabe katika michezo ya kuigiza ya redio ambayo ndiyo ilikuwa burudani ya maelfu ya Watanzania kwa miaka mingi. Mzee Kipara baadaye alianza kuonekana na kujulikana sura zaidi pale alipoanza kuonekana katika michezo iliyoanza kurushwa katika TV, na baadaye katika filamu kadhaa za Kitanzania.

No comments: