Sep 21, 2010

Uzinduzi wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF)

 Umati wa watu waliohudhuria uzinduzi huo

Shirikisho la Filam Tanzania (TAFF) lilizinduliwa rasmi katika viwanja vya Leaders Club siku ya Jumamosi Septemba 18, 2010 na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, wasanii wa filamu na wadau mbalimbali.

Akifungua tamasha hilo Rais wa Shirikisho, Saimon Mwakifamba maaruf kama Jaspa alianza kwa kutoa shukurani kwa serikali kwa kulitambua Shirikisho la Filamu na kazi yao ya kwanza itakuwa ni kutetea maslahi ya wasanii na wadau wote katika tasnia ya filamu kwani mapato wanayopata ni kidogo sana na hayaendani na ugumu wa kazi husika. Vile vile Jaspa alisema kuwa wao kama TAFF wamedhamiria kuanzisha tamasha la filamu litakalojulikana kama Nyerere Film Festival na litaanza mwaka huu litakapofanyika kwa mara ya kwanza hapo Disemba.


Ripoti ya warsha ya TAIPA


Yustus Mkinga, Mtendaji Mkuu wa Cosota

TAARIFA YA WARSHA KUHUSU WIZI WA KAZI ZA SANAA ILIYOFANYIKA UKUMBI WA KITUO CHA UTAMADUNI CHA UFARANSA ALHAMISI TAREHE 19 AGOSTI 2010

Chama cha Watengeneza Filamu na Vipindi vya Luninga na Radio (TAIPA)/UMOJA AUDIOVISUAL E.A. LTD/ na KITUO CHA UTAMADUNI CHA UFARANSA (ALLIANCE FRANCAISE), waliandaa warsha juu ya WIZI WA KAZI ZA SANAA “COPYRIGHT INFRINGEMENT (PIRACY)” iliyofanyika siku ya Alhamisi tarehe 19 Agosti 2010 kuanzia saa 3 asubuhi katika ukumbi wa Kituo cha Utamaduni cha Ufaransa.

Serikali ina dhima ya kuokoa sekta ya filamu-2


Msanii nyota wa kike wa filamu za Bongo, Irene Uwoya

Ninapatashida kidogo kutokana na ukweli kwamba watengenezaji wa filamu wanaoinukia na hata wengi waliopo kwenye soko hili hapa nchini kukosa mfumo mzuri wa kuwawezesha kupata msaada wa mitaji (financials pring board) kwa kazi zao. Hata hivyo, kwa mtazamo wangu, nashauri serikali ijayo kuangalia kwa makini jinsi tunavyoandaa miundo ya kihazina (funding structure) katika kampuni na kazi zetu kabla haijaamua kuelekeza nguvu zake katika kusaidia sekta hii.

Endapo ningepata nafasi ya kuwa mshauri wa Rais katika masuala yanayohusu sekta ya filamu; ningemuomba afikirie sana kuhusu serikali yake kuanzisha mpango maalum wa kutoa mikopo/ruzuku kwa watengenezaji wasinema ambao hawafikiriwi kabisa na mabenki yetu.

Serikali ina dhima ya kuokoa sekta ya filamu


Rais Jakaya Kikwete

Kwanza napenda kumshukuru Rais Jakaya Kikwete kwa angalau kuonesha kuutambua mchango wa sekta ya filamu Tanzania. Hii ni sekta ambayo bado imeonekana kupewa kisogo na hivyo kubaki mikononi mwa wajasiriamali wadogo wasio na mitaji. Haionekani kama nayo inatakiwa kupewa kipaumbele (politicalvaluable) kama sekta muhimu inayoweza kuchangia pato kubwa kwa maendeleo na ukuaji wa uchumi wataifa letu.

Sekta ya Filamu hapa Tanzania haifikiriwi sana kuwa ni taaluma adimu, ndio maana haipewi kipaumbele katika kamati za mipango serikalini. Pia  sekta hii yaweza kuwa mwangamizaji na mchochezi mkubwa katika jamii ya kidemokrasia na pengine kuwa mwasilisha taarifa potofu.