Jun 22, 2016

Kipindi cha XYZ cha Kenya kumilikiwa na Trace TV


Kipindi hiki kinachohitajika sana kimekuwa kikiimarika katika bara Afrika. Mapema mwaka huu kulikuwa na uzinduzi wa Netflix katika soko la Afrika, hatua iliyofurahisha wateja wengi. Hatua hii inajiri wakati ambapo Showmax cha Afrika Kusini kinatarajiwa kuingia katika soko la Kenya. Mipango mengine ni ile ya ushirikiano wa kati ya Airtel na Ericsson kuzindua huduma kwa jina NUVU.

NUVU ilianzishwa nchini Nigeria, hivyo, kuwasaidia wateja kuwa na uwezo wa kuona filamu 3000 za nyumbani na hata kimataifa. Safaricom pia ilikuwa na hamu ya kuanzisha mtandao wa video ikishirikiana na kampuni moja ya India, ‘VuClip’, kuwapatia wateja uwezo wa kuona video katika simu zao kwa shilingi 10 pekee.

Hata hivyo kampuni iliyopata ufanisi mkubwa ni ile ya Buni TV ambayo hutoa video. Mwaka 2012 Buni ilianzisha Video zake na baada ya miezi tisa ilifanikiwa kupata takriban wateja milioni moja. Trace TV sasa imetangaza kwamba inaimiliki Buni TV kama mpango wake wa kuzindua video yake kwa jina Trace Play.

Katika makubaliano hayo,Trace TV imefanikiwa kumiliki haki za runinga na VOD ya vipindi vyote vya Buni vikiwemo ‘Ogas at the top’ nchini Nigeria na XYZ nchini Kenya inayotayarishwa na kampuni mwenza ya Buni Media.

Wafanyakazi wa Kampuni ya Buni TV

Buni TV ilianzishwa na mchoraji vibonzo, Godfrey Mwampembwa, maarufu kwa jina la Gado, ambaye ndiyo mwenyekiti wake. Kampuni hiyo ilikuwa imewaajiri watu 88 wakati ilipouzwa.

No comments: