Jan 16, 2014

Waziri ateua Bodi mpya ya Filamu na Michezo ya KuigizaWaziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara amemteua Mheshimiwa Pindi Chana kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Filamu na Michezo ya kuigiza katika kipindi cha miaka mitatu ijayo. Uteuzi huu unatokana na Mamlaka aliyopewa Waziri huyo chini ya kifungu cha 13(i) cha Sheria ya Filamu na Michezo ya kuigiza Na.4. ya mwaka 1976.

Kwa mujibu wa taarifa ya Wizara hiyo kwa Vyombo vya habari uteuzi wa Mwenyekiti na Wajumbe wengine wa Bodi umeanza tarehe 3 Desemba 2013.Aidha Waziri huyo amewateua Wakili wa Kujitegemea Silvester Sengerema ,Dr. Vicensia Shule kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam na Bishop Hiluka kutoka Shirikisho la Filamu Tanzania kuwa wajumbe wa Bodi hiyo katika kipindi cha miaka mitatu ijayo.

Wajumbe wengine ni Jacob Sarungi kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali , Ntobi Fredrick kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, na Joyce Fissoo ambaye ni Katibu wa Bodi ya Filamu.

1 comment:

Anonymous said...

Kwa kiasi fulani ninafarijika kuona Waziri ameweza kuteua wanaharakati wa ukweli wa masuala ya sanaa. Big up wote mlioteuliwa, mtuwakilishe vema.