Jan 26, 2011

Nini mustakabali wa usambazaji filamu Tanzania? (2)

Cover ya sinema ya Pastor Myamba

Wakati wa upigaji picha za sinema

*Kuhodhi mitandao kama Facebook, Myspace, Youtube, Vimeo ni njia za kujitangaza kwa haraka

WIKI iliyopita nilidokeza kuhusu umuhimu wa maudhui katika filamu, lakini ieleweke kuwa haitoshi tu kuwekeza nguvu kwenye maudhui yanayofaa kama hakuna Jukwaa la Uwasilishaji.
Jukwaa la Uwasilishaji:
Siku hizi, watazamaji wanahitaji pia majukwaa ya habari kama wanavyojali kuangalia maudhui. Falsafa hii ni muhimu wakati unaposhughulikia maudhui yanayowafaa watazamaji. 

Jan 25, 2011

Wasanii wapewa elimu ya sanaa, wahamasishwa kupima UKIMWI

Mkurugenzi Mtendaji wa Parapanda Theatre Lab Trust, 
Mgunga Mwa Mnyenyelwa akiongea kwenye Jukwaa la Sanaa

Baadhi ya washiriki wa Jukwaa la Sanaa

WASANII mbalimbali wakiwemo wacheza filamu, wachoraji, wanamuziki na  wachongaji vinyango na sanamu, Jumatatu wiki hii kwenye Jukwaa la Sanaa wamepata elimu ya sanaa ya maonesho  na kuhamasishwa kupima afya zao na jinsi ya kuepuka kukumbwa na ugonjwa wa ukimwi.

Akizungumza kwenye Jukwaa la Sanaa linalofanyika kila Jumatatu katika ukumbi wa Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), Mkurugenzi Mtendaji wa Parapanda Theatre Lab Trust, Mgunga Mwa Mnyenyelwa, amewataka wasanii wote kuwa na dira katika kazi zao kabla ya kutoa kazi, akawataka wafanye utafiti ili kujua kile wanachokifanya kama kitanufaisha taifa.

Jan 19, 2011

Ushauri kwa wasanii na wadau wa filamu kuunda kundi la ushawishi kwa Serikali watolewa

 Sehemu ya jiji la Dar es Salaam 
ilipofanyika semina ya wadau wa filamu

 Prof. Martin Mhando

Semina iliyowakutanisha wasanii na wadau mbalimbali wa filamu iliyofanyika Ijumaa tarehe 14 Januari kwenye ukumbi wa Kituo cha Utamaduni cha Ufaransa (Alliance Francaise), pamoja na mambo mengine kulikuwa na ushari kwa Wasanii na wadau hao kuunda kundi la ushawishi serikalini ili kuitambulisha serikali umuhimu wa sanaa ya filamu pamoja na muziki.

Ushauri huo wa kuwataka wadau kuunda kundi la ushawishi umetolewa na wataalamu wa mambo ya filamu na sanaa kwa ujumla wakati wa semina hiyo iliyohusu umuhimu wa utamaduni na uchumi kupitia filamu.

Jukwaa la Sanaa lakutanisha Wadau wa filamu na Wasomi

Prof. Amandina Lihamba akiongea kwenye Jukwaa la Sanaa, 
kushoto ni Katibu Mtendaji wa Basata, Gonche Materego

Idara ya Sanaa ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam 
ambapo ni chimbuko la wasomi katika sanaa

Nembo ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam 
wanapotoka wasomi wa kada mbalimbali

Amandina Lihamba na marehemu Kaduma 
kwenye sinema ya Harusi ya Mariam

Jukwaa la Sanaa la Baraza la Taifa la Sanaa la Taifa linalofanyika kila Jumatatu limekuwa kiungo muhimu kwa wadau mbalimbali wa sanaa hapa nchini, Jumatatu hii ya tarehe 17 Januari, 2011 Jukwaa hilo lilishuhudia wasomi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) na waigizaji mahiri katika tasnia ya filamu Tanzania wakijadili kuhusu mustakabali wa Tasnia ya Filamu Tanzania chini ya uratibu wa Profesa Amandina Lihamba.

Nini mustakabali wa usambazaji filamu Tanzania?Msanii na muongozaji wa filamu, Juma Kilowoko (Sajuki)

Flora Mvungi, msanii aliyejizolea umaarufu 
kupitia Bongo Dar es Salaam

KATIKA makala ndefu “Soko la filamu Tanzania linakua?” iliyoisha wiki iliyopita nilidokeza kuhusu tafrani iliyopo kwenye biashara ya usambazaji wa filamu na hujuma zilizopo kutaka kuwaondoa wasambazaji wadogo. Wasomaji kadhaa walinitaka nieleze mtazamo wangu kuhusu mustakabali wa usambazaji filamu badala ya kueleza matatizo yaliyopo tu.

Ili kuelewa mustakabali wa usambazaji filamu, ni muhimu kwanza kuhoji kuhusu yaliyopita. Tunapaswa kuanza kujiuliza: kuna tatizo gani katika usambazaji wa filamu Tanzania?

Jan 11, 2011

Soko la filamu Tanzania linakua? (5)

Tangazo la Sinema ya Aching Heart

Tangazo la vichekesho vya Sharobaro

*Rais anasema linakua kwa kigezo cha filamu zetu kuoneshwa nje ya nchi
*Viongozi wala rushwa wanashirikiana na maharamia wa kazi za sanaa

Nikiwa kama mdau wa filamu na mwanaharakati nalishauri Shirikisho la Filamu Tanzania (Taff) kuonesha meno katika kupigania haki za wanachama wao ikiwa ni pamoja na kuwadhibiti wasambazaji wanaochangia kudorora soko letu.

Jan 7, 2011

SEMINA KUHUSU FILAMU ZA BONGO YAJA


 Prof. Martin Mhando

Ijumaa 14 Jan, 2011, Saa 1:00- 3:00 jioni
Kwenye ukumbi wa Alliance, NI BURE!

BONGO FILMS ZINAELEKEA WAPI?
 
Filamu za Bongo zinazidi kukamata mioyo na akili za Watanzania. Inasemekana kwamba soko la filamu za Bongo sasa limelipiku soko la filamu za Nollywood hapa nchini. Semina hii itajaribu kutoa mwanga juu ya hali halisi ya filamu za Bongo.
 
Profesa Mshiriki Martin Mhando, (Chuo Kikuu cha Murdoch) na Mkurugenzi wa Tamasha la ZIFF, ataongoza jopo la wadau na sinema na watayalishaji wa filamu za Bongo katika majadiliano ya kina ya sinema za Kitanzania na filamu za Bongo.
 

Jan 5, 2011

BASATA yaja na siku ya Msanii

Kazi ya sanaa iliyopo Idara ya Sanaa ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam

 Katibu Mtendaji wa Basata, Ghonche Materego

BARAZA la Sanaa la Taifa (Basata) mwaka huu linatarajia kuandaa Tamasha kubwa la Wasaanii ambalo litakuwa likifanyika kila mwaka likiwa na jina la Siku ya Msanii wa Tanzania.

Katibu Mtendaji wa Basata, Ghonche Materego aliyasema hayo siku ya Jumatatu wiki hii alipokuwa akiwasilisha mada kwenye Jukwaa la Sanaa linalofanyika kwenye ukumbi wa Baraza hilo kila Jumatatu. Gonche alisema kuwa tamasha hilo ambalo litakuwa likipambwa na burudani kemkem kutoka kwa wasanii wa sanaa mbalimbali hapa nchini litakuwa ni maalum kwa ajili ya kuenzi sanaa kwa vitendo.

Watanzania nunueni filamu halisi

Prof. Martin Mhando akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani)

Sharo Milionea, moja ya kazi za Tanzania

MKURUGENZI wa Tamasha la Filamu la Nchi za Jahazi la Zanzibar (Zanzibar International Film Festival), Prof. Martin Mhando, amewataka Watanzania kujitokeza na kununua kazi halisi ili kukuza soko na uchumi wa nchi. Prof. Mhando alitoa wito huo alipozungumza na waandishi wa habari ndani ya ukumbi wa Ngome Kongwe mjini Zanzibar.

Alisema kuwa tayari wasanii wa Tanzania wameweza kupiga hatua katika kutoa filamu mbalimbali, ambazo nyingi kati ya hizo zina mafundisho.

Soko la filamu Tanzania linakua? (4)

Moja ya kazi za Kitanzania, Pretty Girl

Fake Pregnant, kazi nyingine ya Tanzania

*Kulazimisha filamu iwe na sehemu mbili hata kama hadithi hairuhusu siyo haki 
*Kuna hujuma za kuwaondoa wasambazaji wadogo

KWA takwimu za makusanyo “kiduchu” zilizotolewa na serikali kupitia Naibu Waziri nilizozionesha wiki iliyopita, wasanii na watayarishaji wa filamu wa Kitanzania wanapolalamika kunyonywa jasho lao watu wasipende kuwabeza (kwa kisingizio eti hawakusoma na hawazijui haki zao) kwa kuwa kuna matatizo makubwa zaidi ndani ya sekta hii kuliko inavyodhaniwa.

Kwa mfano, unapoongelea suala la usambazaji wa filamu zetu ni jambo linaloumiza sana kichwa. Unapokutana na mtayarishaji wa filamu hapa nchini ukaongea naye kuhusu biashara ya uuzwaji/ usambazaji wa filamu unaweza kulia, jinsi biashara inavyojengewa mazingira ya kuwa ngumu kuliko biashara nyingine yoyote.

Jan 4, 2011

Filamu za This is it na Huba kuoneshwa tamasha la Fespaco- Ouagadougou

 Steven Kanumba
 Ahmed Ulotu maaruf kama Mzee Chilo
Filamu mbili za Kitanzania: “This is it” ya Steven Kanumba na “Huba” ya Ahmed Olutu, zimefanikiwa kutwaa tuzo ya filamu bora katika tamasha dogo (Min Ziff) la nchi za jahazi Zanzibar, lililomalizika kisiwani juzi.
Mwenyekiti wa Ziff, Hassan Mitawi aliwapongeza wasanii na waandaaji wa filamu hizo kwa kutumia uwezo mkubwa kwa kuwa filamu hizo zimeonekana kuwa na mvuto wa kipekee na ana uhakika filamu zilizoshinda zitaenda kuwakilisha vyema Tanzania kwenye tamasha la Fespaco. Aidha, tuzo ya muigizaji bora wa filamu wa tamasha hilo,