Amil Shivji
TAKRIBAN
wiki mbili zilizopita nilikuwa mjini Bujumbura nchini Burundi kwa mwaliko wa
Shirika la Kijerumani la GIZ, ambapo Mtandao wa Wanafilamu wa Afrika Mashariki
ulikuwa ukizinduliwa rasmi, sambamba na Tuzo za filamu kwenye Tamasha la
Kimataifa la Filamu la Burundi (Festicab) 2014, linalofanyika jijini Bujumbura.
Kabla
ya safari yangu hii, nilipata bahati ya kupitia nchi zingine kama mbili ambapo
nilipata nafasi ya kukutana na watengeneza filamu wa nchi hizo, na kwa kweli
nilijifunza mengi kutoka kwao.