Jan 25, 2012

Tungetumia filamu, nyimbo zetu kuhamasisha uzalendo

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Emmanuel Nchimbi akiwa na wajumbe wa kamati ya kutafuta vazi la taifa, ofisini kwake jijini Dar es Salaam

MWAKA jana tumetimiza miaka 50 tangu tuwe huru, lakini bado jamii ya Kitanzania imeendelea kupoteza maadili, mila na tamaduni zake kila kukicha. Baada ya uhuru wa Tanganyika mwaka 1961, Wizara ya Utamaduni wa Taifa na Vijana iliundwa mwaka 1962, rais wa wakati huo, Mwalimu Julius Nyerere, ambaye alitamka wazi kuwa Utamaduni ndiyo kiini na roho ya Taifa, na nchi inayokosa utamaduni wake ni sawa na mkusanyiko wa watu usiokuwa na roho na hivyo kukosa sifa ya kuitwa taifa kamili.



Miaka hii hamsini ya uhuru tunazidi kushuhudia mmomonyoko mkubwa wa maadili huku tasnia ya sanaa hapa ikionekana kutelekezwa kabisa na serikali yetu bila kujali kuwa tasnia hii imesheheni utajiri mkubwa ambao ungeliingizia taifa hili mapato,

Jan 24, 2012

Swahiliwood - Part 1 - An Introduction




Ilikuwa ni  Jumanne ya tarehe 22 Novemba hadi Jumamosi tarehe 26 Novemba, warsha ya siku tano ambayo ni ya kwanza katika mkakati maalum uliowekwa na taasisi ya Media for Development International – Tanzania (MFDI-Tanzania), kuhakikisha kuwa tasnia ya filamu nchini “Swahiliwood” kama ambavyo wanapenda ijulikane, inafikia kile ambacho tasnia zingine duniani zimeweza.


Washiriki 25 walihudhuria warsha hiyo, wakiwemo watayarishaji wa filamu maarufu na waandishi maarufu wa script. Mimi nilikuwa mmoja wao. Washiriki wengine maarufu waliohudhuria ni pamoja na Jacob Steven (JB), Mahsen Awadhi (Cheni), Suzanne Lewis (Natasha), George Tyson, Hamisi Kibari, John Lister, Ali Yakuti (ambaye hakumaliza mafunzo), Ali Mbwana (Bashiri Mpemba), Chrissant Mhengga na wengineo.

Jan 19, 2012

KANUNI ZA BODI: Waziri Nchimbi, ni busara zako tu ndio zitamaliza mgogoro huu

*Vinginevyo tutarajie yaliyotokea Nigeria

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo,
Dk Emmanuel J. Nchimbi

Muigizaji wa Nigeria, Desmond Elliot

Tasnia ya Filamu ya Nigeria

NOLLYWOOD imekufa! Imekufa kwa sababu ya viongozi waliopewa dhamana ya kuilinda na kulinda maadili kujiingiza katika kuanzisha miradi ya kukusanya mapato bila hata kujali itaathiri vipi soko la filamu la nchi hiyo. Fikiria, kwa sekta ya filamu iliyokuwa inatengeneza sinema mia moja kila mwezi katika siku za nyuma, hivi sasa haiwezi hata kutengeneza sinema saba katika mwezi! Hapa lazima kuna tatizo kubwa; 7/100!  Hakika huko ni kushindwa!



Nollywood kumebakia watu wachache kama Desmond Elliot, Uche Jumbo, Monalisa Chinda, Stephanie Okereke, Emem Isong na wengine wachache wanaojaribu kutoa sinema. Wao wanajaribu kupambana kama mtu mmoja mmoja.

Jan 13, 2012

Hatimaye gwiji wa maigizo, Mzee Kipara azikwa jijini Dar es Salaam

Picha zilizopo juu zinawaonesha baadhi ya wasanii na wananchi waliojitokeza kumzika Mzee Kipara, wengine wakiwa wamebeba jeneza wakati wa kuelekea Makaburi ya Kigogo, Jijini Dar es Salaam

Baadhi ya waumini wa Kiislam walifanya ibada ya kusalia maiti ya Marehemu Mzee Said Fundi eneo alilokuwa akiishi la Kigogo jijini Dar es Salaam

Maelfu ya wakazi wa jijini la Dar es Salaam na vitongoji vyake, jana Alhamisi walijitokeza katika mazishi ya msanii mkongwe wa sanaa ya maigizo, Fundi Said maarufu kwa jina la Mzee Kipara aliyefariki dunia katika nyumba aliyokuwa amepangishiwa na Kundi la Sanaa la Kaole iliyopo Kigogo Mbuyuni, Dar es Salaam.

Mzee Kipara, alikuwa msanii mkongwe katika tasnia ya uigizaji Bongo, aliyetumia sehemu kubwa ya maisha yake katika sanaa ambaye juzi (Jumatano), Januari 11, mwaka huu, saa 2:00 asubuhi, Mungu alimchukua baada ya maumivu ya muda mrefu.

Jan 11, 2012

Mzee Kipara hatunaye tena...

Mzee Said Fundi enzi za uhai wake

Picha hii inamuonesha alipokuwa anaumwa


Mzee Said Fundi, aliyekuwa maarufu kama Mzee Kipara, msanii ambaye amedumu katika sanaa kwa miaka mingi sana amefariki dunia asubuhi saa mbili leo Jumatano tarehe 11 Januari, 2012. Mwanaharakati na mwanamuziki wa siku nyingi, John Kitime, anasema alimfahamu Mzee Kipara kwanza akiwa mwigizaji katika magazeti ya picha yaliyokuwa yakiitwa FILM TANZANIA, baadaye walikutana 'live' akiwa TT katika treni ya reli ya kati.

Jan 4, 2012

Bado tuna kazi kubwa ya kurudisha maadili

Katibu Mtendaji wa Bodi, Joyce Fisso

Msanii Elizabeth Michael, maaruf kwa jina la Lulu

SIKU ya Jumanne ya wiki hii kulikuwa na mjadala kuhusu maadili katika filamu za Tanzania uliorushwa na kituo cha redio (Radio One), mjadala ambao uliwahusisha, Rais wa shirikisho la filamu nchini, Simon Mwakifwamba, mwakilishi kutoka Bodi ya Ukaguzi wa Filamu na mwananchi mmoja aliyewakilisha watazamaji wa filamu. Wadau hawa walipata nafasi ya kuchangia maoni yao kulingana na mitazamo yao. Kwa kweli sikupata kabisa bahati ya kusikia hoja zao kwa kuwa sikuwa na taarifa kama kungekuwa na kipindi kama hicho, nilipata taarifa wakati kipindi kikiwa kimekwisha na sikuweza kujua waliongea nini.



Lakini pamoja na hayo, bado hainizuii kutoa maoni yangu kuhusiana na jambo hili la maadili kwa kuwa naamini kuwa bado ipo haja kwa wadau wote kutafuta njia bora ya kutatua matatizo yaliyopo katika tasnia na soko la filamu nchini.