Marehemu Dalillah Peter Kisinda (Tabia)
Kava la filamu ya Naomi (part 2)
TASNIA ya filamu nchini mwetu imezidi kukua na kuendelea kuua soko la filamu kutoka Nigeria ambazo mwanzoni mwa miaka ya 2000 zilikuwa zimeliteka soko la nchi yetu. Tofauti na ilivyokuwa miaka michache iliyopita, kwa sasa takriban, filamu mbili mpya za Kitanzania hutoka kila wiki na hali inaonesha kwamba idadi hiyo itazidi kupanda miaka michache ijayo, hasa kama watengeneza filamu wa Tanzania wataboresha zaidi kazi zao.
Moja ya filamu inayosubiriwa kwa hamu ni ya Naomi, iliyotayarishwa na mmoja wa Watunzi mahiri wa hadithi nchini na mtengeneza filamu, Hamisi Kibari.